Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yatoa vifaa tiba Hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere

CT Scan Of Brain Hero Serikali yatoa vifaa tiba Hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere

Thu, 23 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkoa wa Mara umepokea vifaa tiba vya zaidi ya Sh4.8 bilioni kwaajili ya Hospitali ya Rufaa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere pamoja na Sh232 milioni kwaajili ya ununuzi wa vifaa tiba kwenye kituo cha afya cha Kisorya wilayani Bunda.

Mbali na vifaa hivyo pia umepoekea magari 20 ya wagonjwa (Ambulence) pamoja na magari 11 kwaajili ya ufuatiliaji wa huduma za afya na miradi mbalimbali ya afya.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Novemba 22, 2023 Mkuu wa Mkoa wa Mara, Said Mtanda amesema vifaa hivyo vitasaidia kuboresa huduma za afya zinazotolewa na vituo vya umma.

Ametaja baadhi ya vifaa vilivyopokelewa ni mashine ya C-T Scan, mashine ya kusafisha damu, Ultra Sound, mashine ya kushtua moyo na vipimo vya maabara.

"Wananchi walikuwa wakipata wakati mgumu kupata huduma na mara nyingi walikuwa wakilazimika kupewa rufaa kwenda Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kwahiyo ujio wa vifaa hivi ni nafuu kubwa kwa wananchi,”

"Kwa vifaa hivi kila halmashauri itapata magari mawili ya wagonjwa, gari moja la ufuatiliaji hivyo kusaidia kupunguza changamoto za huduma za afya katika halmashauri zetu kwa manufaa ya jamii nzima," amesema

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara, Dk Zabron Masatu amesema Sh232 milioni kilichoelekezwa kwenye kituo cha afya cha Kisorya kitasaidia ununuzi wa vifaa tiba hasa upande wa mama na mtoto.

Amesema Mkoa wa Mara bado unakabiliwa na changamoto ya vifo vya watoto wachanga ambapo mwaka jana watoto 700 walifariki dunia hivyo uboreshaji wa huduma za afya hasa za mama na mtoto ni jambo la muhimu.

"Kwa mwaka huu hadi sasa watoto 500 wamefariki dunia hivyo Serikali baada ya kuona hali hii imeamua kuwekeza kwa kujenga majengo na vifaa tiba ambapo kwa kuanzia tumeona fedha hizi zielekzwe Bunda huku tukitafuta fedha kwaajili ya maeneo mengine,"amesema

Kuhusu Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Dk Masatu amesema ilikuwa ikikabiliwa na changamoto ya upungufu wa vifaa hivyo hali ambayo mbali na kuwapa wakati mgumu katika kutoa huduma lakini pia ilikuwa kero kwa wananchi.

"Tunakuwa na wastani wa mgonjwa mmoja kila siku anayehitaji huduma ya CT Scan na kwavile hatukuwa na kifaa tulikuwa tunalazimika kuwapa rufaa wagonjwa kwenda Bugando na tuna wastani wa wagonjwa 6 kwa wiki wanaohitaji huduma ya kusafishwa damu kwahiyo unaweza kuona namna ambavyo vifaa vitasaidia," amefafanua

Baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Musoma wameishukuru serikali kwa vifaa hivyo kwa maelezo kuwa vitasaidia kupumguza gharama kubwa walizokuwa wakizipata kutafuta huduma.

"Mimi nilitaka huduma ya CT- Sacn mwezi uliopita nikalazimika kwenda Bugando nilitumia gharama kubwa na muda mwingi kupata huduma, niipongeze Serikalikwa hatua hii"amesema Amos Chitara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live