Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yatoa tamko kuhusu majengo marefu kutitia Dodoma

P 6849574358474522561912 0 789421c8bdd82127531e0f8f7fbf5f29 Serikali yatoa tamko kuhusu majengo marefu kutitia Dodoma

Tue, 14 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imesema haijawahi kutangaza kuwa mkoa wa Dodoma haufai kujengwa majengo marefu kwa sababu ya kutitia kama ilivyokuwa ikivumishwa na watu ambao hawakuwa na taarifa rasmi. 

Hayo yamebainishwa juzi tarehe 12 Februari 2023 na Afisa Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), Dk. Matiko Mturi alipokuwa akiongea na waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya baraza hilo katika mkutano na vyombo vya habari katika ukumbi wa Habari Maelezo Jijini Dodoma.

Akijibu maswali ya wanahabari muda mfupi baada ya kuwasilisha taarifa yake ya utekelezaji alisema kuwa si kweli kuwa Jiji la Dodoma haufai kujengwa majengo makubwa na marefu bali ni suala la upangaji wa makazi ambao unafanywa na jiji husika.

“Kumekuwepo na uvumi kuwa Dodoma haistahili kujengwa majengo marefu kutokana na kuwa na maji mengi chini kutokana na kuwepo kwa kauli hiyo wewe ukiwa mshauri na mtendaji wa baraza la taifa la ujenzi unatoa kauli gani ili tuweze kuwa na uhakika wa hizi kauli au kuwahabarisha wananchi ambao wengine wanaweza kuwa na hofu,” aliuliza mmoja wa wanahabari.

Akijibu swali hilo Dk. Mturi amesema kuwa siyo kweli kuwa Dodoma haistahili kujenga majengo marefu, ila kila sehemu uweza kujengwa kulingana na teknolojia ya eneo husika.

“Nataka kujua nani aliyewahi kusema kuwa Dodoma haiwezi kujengwa majengo marefu wala makubwa isipokuwa kama kuna sehemu yenye matetemeko basi ujenzi ufuata teknologia iliyopo na iwapo majengo ujengwa kwa ukanda utegemea mpangilio wa halmahauri au majiji kwa nia ya mpangilio wa kupendezesha mji kwa maana ya kuamua kuwa ni wapi yajengwe magorofa, nyumba fupi au nyumba za aina fulani,” amefafanua Dk. Mturi.

Akizungumzia majukumu ya baraza amesema kuwa baraza linatekeleza majukumu tisa ambayo ameyataja kuwa ni kukamilisha mwongozo wa gharama za ujenzi wa barabara nchi nzima kwa kuandaa gharama za msingi za makandarasi katika kutekeleza kazi mbalimbali za ujenzi wa barabara kwa kila mkoa Tanzania Bara.

Ametaja majukumu mengine kuwa ni kuandaa mapendekezo ya kuboresha sheria na miongozo inayosimamia ujenzi wa majengo nchini.

Aidha, amesema kuwa viwango mswazo ya majengo ya serikali, kutoa mafunzo kujenga uwezo wa wadau wa sekta ya ujenzi nchini, kutoa fahirisi za bei za vifaa, mitambo na ujura katika shughuli za ujenzi kwa kila mwezi ili kuonesha mabadiliko ya bei ya vifaa vya ujenzi na mambo mengine.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live