Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yatoa mabilioni kukarabati miundombinu Lindi

Fedhapic Serikali yatoa mabilioni kukarabati miundombinu Lindi

Fri, 3 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mvua kubwa za El-Nino zilizonyesha zimeleta athari maeneo mbalimbali hapa Nchini ikiwemo katika Mkoa wa Lindi ambapo zimesababisha uharifu mkubwa wa miundombinu ya barabara na madaraja.

Mvua hizo katika baadhi ya maeneo zilikwamisha shughuli za maendeleo ya Wananchi, na hivyo kuifanya Serikali kupitia Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) kufanya kila linalowezekana kurejesha mawasiliano ya barabara zilizokatika kwa haraka.

Kwa kuliona hilo, Serikali ya awamu ya sita chini ya Dk. Samia Suluhu Hassan imetoa shilingi bilioni 5 ambazo ni fedha za dharura kwajili ya kurejesha miundombinu ya barabara na madaraja ambayo imeharibika katika Mkoa wa Lindi.

Meneja wa TANROADS Mkoa wa Lindi Mhandisi Emil Zengo ameyasema hayo tarehe 2 Mei 2024; alipotembelea kukagua hatua za ujenzi zinazoendelea katika daraja la Somanga linalounganisha Mikoa wa Dar es Salaam - Pwani, Lindi, Mtwara na Ruvuma ambalo lilikatika kutokana na mvua za El-Nino na kusababisha magari ya abiria na mizigo kukwama njiani.

Amewataka Wananchi wanaoishi karibu na barabara kuacha kufanya shughuli za kibinadamu kwenye kingo za barabara pamoja na kutupa taka ngumu katika mitaro kwani kufanya hivyo kunasababisha maji kushindwa kupita pindi mvua zinaponyesha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live