Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yatoa Sh38 bilioni za miradi ya maendeleo Kilosa

Mwakapicc Data Serikali yatoa Sh38 bilioni za miradi ya maendeleo Kilosa

Sun, 13 Mar 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Katika kipindi cha mwaka mmoja Serikali imetoa Sh38 bilioni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya afya, elimu, maji, mawasiliano na miundombinu.

Hayo yalisemwa jana na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Alhaji Majid Mwanga wakati akielezea mafanikio ya mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan,

Alhaji Mwanga amewata watendaji na viongozi wote wa Halmashauri hiyo kufanya kazi kwa bidii, kuonesha uadilifu na uamnifu hasa katika matumizi ya fedha za miradi hiyo ya maendeleo.

Hivyo amewataka Wananchi wa wilaya hiyo kumuunga mkono Rais Samia katika mambo mbalimbali ya kitaifa ikiwemo usajili wa anuani za makazi, sensa na chanjo kujikinga na Uviko-19.

"Wale watakaoharibu ama kuiba miundombinu ya barabara, reli ama vibao vya kuonesha mitaa na barabara vitakavyowekwa hivi karibuni nitakula nao sahani moja na nitahakikisha wanashughulikiwa," amesema Alhaji Mwanga.

Katika hatua nyingine Alhaji Mwanga amewataka watendaji wa kata na vijiji kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka huu wanafika shule na kuendelea na masomo.

Advertisement Kwa upande wake Mbunge wa Kilosa Kati, profesa Palamagamba Kabudi amesema fedha zilizoletwa na Serikali katika katika kipindi cha uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan zimeboresha sekta mbalimbali ikiwemo ya mawasiliano kwani jumla ya minara 12 imejengwa katika vijiji ambavyo vilikuwa havina huduma ya mawasiliano ya simu.

"Muda si mrefu Wilaya ya Kilosa itakuwa na heshima kubwa kwani Tarura iko kwenye mipango ya kuboresha na kujenga barabara zitakazounganisha vijiji, kata na mikoa ya jirani ikiwemo ile ya kutokea Melela, Mkata, Palakuyo, Kimamba, Chanzulu, Kilosa hadi Mikumi na hatimaye barabara hiyo kuelekea mikoa ya Iringa na Mbeya," amesema Profesa Kabudi

Chanzo: www.mwananchi.co.tz