Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yatoa Sh13.5 bilioni miradi ya maendeleo ya Polisi

Poilisi Miradi Maendeleo Serikali yatoa Sh13.5 bilioni miradi ya maendeleo ya Polisi

Tue, 4 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imetoa zaidi ya Sh13.5 bilioni kwaajili ya miradi ya maendeleo ya Jeshi la Polisi nchini mwaka 2021 ambapo miradi hiyo inajumuisha ujenzi wa baadhi ya ofisi za makamanda wa polisi mikoa na nyumba za kuishi askari.

Fedha hizo zimetolewa na serikali kupitia tozo za miamala ya simu katika kipindi hicho ambapo miongoni mwa majengo ya ofisi za makamanda  wa polisi zilizonufaika ni pamoja na mkoa wa kipolisi wa Tarime/Rorya pamoja na mkoa wa Mara.

Akizungumza baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa jengo la makao makuu ya jeshi hilo Tarime/Rorya Jumatatu, Oktoba 3, 2022 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini amesema kuwa hatua hiyo inalenga kuboresha utendaji kazi wa jeshi hilo.

“Ni kweli kuna baadhi ya ofisi za makamanda kama hapa Tarime/Rorya hazina hadhi na hali hii imekuwa ni miongoni mwa sababu zinazoshusha morali ya utendaji kazi wa vijana wetu.

“Sasa serikali imeamua kuwa lazima iboreshe mazingira ya utendaji kazi kwa vijana wetu hawa ili kazi zifanyike kwa ufanisi," amesema

Amelitaka jeshi hilo kuhakikisha kuwa linapambana na vitendo vya uhalifu ili nchi iwe salama muda wote hali ambayo pia itapelekea watanzania wote kwa ujumla kushiriki katika shughuli za kiuchumi na kijamii kwa uhakika.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Tarime/Rorya, Godfrey Sarakikya amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa mkoa huo wa kipolisi mwaka 2009, askari polisi wamekuwa wakipata wakati mgumu katika utendaji wao wa kazi kutokana na ukosefu wa ofisi na nyumba za makazi.

"Ofisi ya RPC ipo katika jengo la kupanga la chama cha ushirika na licha ya jengo hilo kuchoka, kodi yake pia imekuwa ikipandishwa mara kwa mara.

“Tunashukuru serikali kwa mradi huu na pia tunaomba tuongezewe miradi mingine ili tuweze kutatua changamoto ya makazi na ofisi kwa ujumla," amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live