Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yatenga miezi minne kuwahamisha wakazi Ngorongoro

Maasai Boma In Ngorongoro Conservation Area Serikali yatenga miezi minne kuwahamisha wakazi Ngorongoro

Mon, 17 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imepanga kutumia muda wa miezi minne mfululizo katika zoezi la hiari la kuwahamisha wakazi wanaoishi maeneo ya Hifadhi ya Ngorongoro Mkoani Arusha kuelekea Katika Makazi mapya ya kudumu katika Kijiji cha Msomera wilayani handeni Mkoani Tanga baada ya zoezi hilo kusimama kwa muda.

Akiongea Waziri wa Maliasili na Utalii Mohamed Mchengerwa baada ya Kuwasili katika Ofisi za Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Zilizoko Mkoani Arusha na Kufanya Ziara yake ya kwanza tangu ateuliwe katika nafasi hiyo ya kukagua Miradi ya Maendeleo Hifadhini humo ambapo amewapongeza Wananchi hao kwa kuzidi kujitokeza kujisajili kwa hiyari kwa ajili ya taratibu za kuhama katika makazi mapya ya Kijiji Cha Msomera,huku akiwahimiza kuendelea kushirikiana na Serikali ili kukamilisha zoezi

Inatajwa hadi kufikia Januari 11.2023 jumla ya kaya 1524 zenye watu 8715 na mifugo 32,842 wameshajiandikisha kwa ajili ya kuhama kwa hiari.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live