Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amesema, katika kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, jumla ya miradi 717 imetekelezwa mkoani humo kwa gharama ya zaidi ya shilingi Bilioni 620.
Babu amesema miradi hiyo 717 imetekelezwa katika sekta za afya, elimu, miundombinu ya barabara, maji, kilimo, mifugo, usafirishaji na uchukuzi, mipango miji pamoja na uwezeshaji wa Wananchi kiuchumi.
Mkuu huyo wa mkoa wa Kilimanjaro ameyasema hayo alipokuwa akihutubia kongamano la kuangazia maendeleo ya miradi inayoendelea kutekelezwa na iliyotekelezwa katika kipindi cha miaka miwili ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa mkoa wa Kilimanjaro.