Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yataka uwajibikaji udhibiti mimba, ndoa za utotoni

Child Marriage Facts And How To Help Girl Facing Away Serikali yataka uwajibikaji udhibiti mimba, ndoa za utotoni

Fri, 20 Jan 2023 Chanzo: dar24.com

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Batilda Buriani ameagiza ya kuongezwa kwa uwajibikaji katika usimamizi na utekelezaji wa mipango mikakati itakayoandaliwa, ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na watoto wachanga, kudhibiti mimba na ndoa za utotoni.

Batilda ameyasema hayo katika ufunguzi wa kikao cha watalaam wa Afya Kanda ya Magharibi, inayounda mikoa ya Tabora, Katavi na Kigoma cha kujadili mikakati ya kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na watoto wachanga katika kanda hiyo.

Amesema, Kiwango cha mimba za utotoni kwa kanda ya Magharibi ni asilimia 25.2 kwa Mkoa wa Katavi, Tabora asilimia 17 na Kigoma asilimia 11.9 huku hudhurio la kwanza la wajawazito chini ya wiki kumi na mbili kwa mkoa wa Tabora likiwa ni asilimia 34.4, Katavi asilimia 41 na Kigoma asilimia 54.9.

Mkuu huyo wa Mkoa, amefafanua kwamba kiwango cha utumiaji wa njia za kisasa za uzazi wa mpango kwa mkoa wa Katavi ni asilimia 41, Kigoma asilimia 46.4 na Tabora asilimia 60.1 hivyo kutaka elimu ya Afya itolewe kwenye jamii.

Aidha ameongeza kuwa, elimu hiyo itolewe kupitia njia mbalimbali za mikusanyiko ya watu, mashuleni, makanisani na misikitini, vyombo vya habari na kwamba wale wote wanaowapa mimba watoto wa shule sheria ichukue mkondo wake, ili kudhibiti vitendo hivyo.

Chanzo: dar24.com