Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yataja maeneo hatari kwa kipindupindu Dar

Uchafu Dar Serikali yataja maeneo hatari kwa kipindupindu Dar

Mon, 15 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mohammed Mang'una ametaja maeneo hatarishi zaidi yenye uwezekano wa kupata mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu huku akiwataka wananchi wachukue tahadhari.

Dk Mang'una ameyataja maeneo hayo leo, Jumatatu Januari 16,2023 katika mkutano wa Mkuu wa Mkoa, Albert Chalamila na watendaji wa Serikali kuhusu tahadhari dhidi ya magonjwa ya mlipuko.

Tayari Serikali imetaja mikoa sita ambayo ugonjwa huo upo hadi sasa lakini wa Dar es Salaam haupo na tayari wagonjwa 318 wameripotiwa kuanzia Septemba mwaka jana.

Akitoa taarifa ya hali ilivyo kwa Mkoa wa Dar es Salaam na tahadhari walizozichukua katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo, Mganga huyo aliyataja maeneo ambayo ni Kwa Mnyamani Tabata, Vingunguti, Mwananyamala, Tandale, Kigogo, Makumbusho, Hananasif, Msasani, Kunduchi na Magomeni, Azimio, Keko, Tandika, Yombo Vituka, Charambe, Machangarawe, Mtoni, Mbagala na Buza aidha pia kuna maeneo ya Mburahati, Manzese, Ubungo, Mbezi, Goba, Kigamboni,Mji mwema, Vijimbweni na Kibada

Kuhusu hatua ambazo wamezichukua mpaka sasa amesema ni maoja na kutenga kambi katika Halmashauri zote, vituo viwili kwa ajili ya mawasiliano na maafa na kuongoza idadi ya maofisa afya ikiwemo katika kituo cha mabasi ya mikoani cha Magufuli.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live