Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yashughulikia tatizo la maji Dar

Majimji Serikali yashughulikia tatizo la maji Dar

Mon, 31 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kutoka kwenye ukurasa rasmi wa mtandao wa instagram wa Waziri wa Maji @jumaa_aweso;

“Jioni hii Nimefika kwenye Tenki letu la KISANGA Wazo Baada ya kukamilisha kazi kubwa sana ya marekebisho ya Bomba kubwa kuongeza msukumo wa Maji kwa mkoa wa Dar Es Salam leo nimeshuhudia Kazi ya ujazaji wa tank la Maji Kisanga lililopo eneo la Wazo tangu mchana nankukamilika sasa.

Tanki hili linahudumia wananchi wa maeneo ya *Mbezi Beach A, Mbezi Beach B, Tegeta Msichoke,Bahari Beach, Kunduchi, Mtongani, Kiaroni, Madini, Meko, Africana,Kawe, kuelekea Mikocheni viwandani.

Baadhi ya maeneo ya jirani ikiwemo Tangi bovu huduma imekwishaanza kupatikana na itaendelea kupatikana hatua kwa hatua na mafundi wetu wapo mitaani kwa kazi ya kutoa upepo kwa maeneo mabomba yaliyoziba kwani kumekosa maji kwa muda.

Kesho (Oktoba 31,2022) tutaruhusu Maji ya Tenki la Chuo, ambapo huduma itafika Mikocheni, Mwenge, Kinondoni, Mwananyama, Mlalakua, Namanga, Msasani, Masaki, Osterbay, Upanga, Kariakoo, Gerezani, Keko, Chang’ombe, Mivinjeni, Kilwa road mpaka uhasibu na baadhi ya maeneo ya Sinza kwa operation maalum.

Ni bayana matengenezo haya ambayo ilikua lazima tuyafanye ili kukabiliana na kina cha maji kilichochini sana kwasasa yameathiri pia ratiba ya mgao wetu na sasa baada ya kazi hii kukamilika tunaweza kurejea kwenye mstari.

Kwa maeneo mengine kama vile Temeke Magorofani, Wailesi, Changombe, Mivumoni- Bucha, Faraja Chabwela na Ilasi pia yalipata maji.

Maeneo mengine ni Kibamba Hondogo, Kiluvya kwa Komba, Madukani, Butiama, Kwembe Mpakani King’azi B, Kiluvya kwa Sumaye hadi Kifai.

Jioni hii, maji yameanza kutoka Kimara Matangini, Mtingwa, Bonyokwa na maeneo ya Suca.

Niendelee kuwatia moyo wataalamu na mafundi wetu wanaoendelea kupambana usiku na mchana wasichoke na kama kiongozi wao nathamini mapambano wanayoendelea nayo.

Kwa wananchi tunaendelea kuwaomba sana radhi kwa hali hii huku tukiwasihi kuendelea kuwa wavumilivu katika nyakati hizi ngumu.

Wiki ijayo tutaruhusu maji toka Visima vyetu virefu vya Kigamboni kwaajili ya eneo la Kigamboni na kuingia mjini Dar Es Salaam na punde tutawapa taarifa ya utiaji saini wa Mradi wa ujenzi wa Bwawa la Kidunda mwezi Novemba"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live