Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yapiga marufuku wanafunzi yatima kufukuzwa shule kwa kukosa ada

Bdc568fcbdc7119e6761e7ebae31771a Shule za St.Anne Marie zatii agizo la kutowarudisha nyumbani wanafunzi

Mon, 27 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa shule ya St. Anne Marie Academy, umetii agizo la Serikali la kutowafukuza wanafunzi shule pindi wazazi wanapochelewa kulipa ada katika muda muafaka uliowekwa na shule iyo.

Wamefikia uamuzi huo baada ya Waziri wa Elimu, Prof, Joyce Ndalichako kusisitiza shule binafsi kutowarudisha nyumbani wanafunzi kwa kigezo cha ada.

Mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi wa shule hizo, Dk Jason Rweikiza, alitangaza kuhusu kusitisha suala la wanafunzi kurudishwa nyumbani kwa kushindwa kulipa ada kwa sababu mbalimbali kama vifo vya wazazi.

Ameongeza kusema kuwa kwa mwaka 2021 shule hizo zimepoteza wazazi 93 jambo ambalo limefadhaisha malipo ya ada ya watoto na kupelekea wengine kuacha masomo yao

"Tumekuwa tukipoteza wazazi wengi kila mwaka na katika mwaka huu wa 2021 pekee, tumepoteza wazazi 93 na hii inarudisha nyuma ufaulu wa masomo kwa watoto kwani wengi wao hawana uwezo wa kulipa ada ya shule, lakini kuanzia leo, ninatangaza hakuna mwanafunzi atarudishwa nyumbani baada ya kifo cha mzazi wake, Ikiwa mwanafunzi yuko Darasa la Kwanza, ataendelea hadi Darasa la Saba na ikiwa yuko Kidato cha Kwanza ataendelea na Kidato cha Nne bila kukatishwa," Amesema Mkurugenzi huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live