Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yaondoa sharti la wenye ulemavu kupata mikopo

Jastina Waziri Jenista Mhagama

Thu, 16 Sep 2021 Chanzo: Mwananchi

Serikali imeondoa sharti kwa watu wenye ulemavu kuunda kikundi ili wapate mkopo wa wa asilimia 10 unaotolewa na halmashauri nchini kwa kundi hilo pamoja na lile na wanawake na vijana.

Badala yake, mtu mmoja mwenye ulemavu atakuwa na uwezo wa kuchukua mkopo bila kutegemea kikundi chochote jambo ambalo litawapa fursa zaidi ya kupata fedha na kuendelea shughuli zao mbalimbali.

Kuondolewa kwa sharti hilo kumetokana na malalamiko wenye ulemavu ya kushindwa kunufaika na fursa hiyo kutokana na kukosa kikundi chenye watu zaidi ya watano chenye malengo yanayofanana

Hayo yamesemwa Alhamis Septemba 15,2021 na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama alipokutana na wenye ulemavu.

Mhagama amesema wabunge waliamua kuhakikisha asilimia 10 ya mapato ya halmashauri yanayotolewa kwa ajili ya mkopo, asilimia mbili ya fedha hizo lipewe kundi hilo kama mkopo lakini haikuw aikiwafikia kama ambavyo ilitarajiwa.

“Serikali kupitia Bunge, Tamisemi (Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) ikaamua kuondoa sharti la lazima muwe kwenye vikundi kwa hiyo mtu mwenye ulemavu ana uwezo wa kupata mikopo hata kama akiwa mwenyewe,”amesema

Chanzo: Mwananchi