Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yaombwa kuingilia kati mgogoro wa ardhi

Diwani Mgogoro Serikali yaombwa kuingilia kati mgogoro wa ardhi

Tue, 8 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Magu mkoani Mwanza wameiomba serikali kuingilia kati mgogoro wa ardhi uiliopo katika kijiji cha Kanyama kata ya Kisesa baada ya familia tatu kubomolewa nyumba na kuporwa ardhi na mwekezaji bila kupata fidia yoyote.

Kauli hiyo wameitoa kwenye kikao cha baraza la madiwani cha kupitia miradi ya maendeleo kwa kipindi cha robo ya kwanza mwezi July hadi September mwaka huu, ambapo wamesema kumekuwa na migogoro ya ardhi isiyoisha ambayo imekuwa ikiwaumiza wananchi na kuwaacha wakihangaika kwa kuporwa ardhi na wawekezaji na kumtaka Mkurugenzi kufuatilia migogoro hiyo na kuipatia ufumbuzi.

Akilitolea ufafanuzi suala hilo la mgogoro wa ardhi Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Merchandus Lusasa amewaahidi madiwani hao kufuatilia mgogoro huo huku Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo ya Magu Mpandalume Hondola akitaka majibu yapatikane haraka vinginevyo baraza litachukua hatua kali za kisheria

‘Sasa hilo ni suala la kitaalamu litafanywa na menejimenti na kama mheshimiwa mmoja alivyoomba litaenda kwenye kamati na haki itapatikana kwahiyo tulifanyie kazi kuliko kulipa sura tofauti tofauti tunaweza kufika kwenye hitimisho lisilo sahihi.’ Amesema Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Merchandus Lusasa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live