Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yaombwa kuboresha miundombinu ya elimu

Untitled 1 6 Serikali yaombwa kuboresha miundombinu ya elimu

Mon, 16 Jan 2023 Chanzo: eatv

Ili kuleta utulivu na ufanisi wa kazi ya ualimu katika utekelezaji wa majukumu yao, Chama cha walimu wilayani Kiteto mkoani Manyara, kimeomba serikali kuboresha miundombinu ya elimu sambamba na ujenzi wa nyumba za waalimu, kuboresha Sekta hiyo .

Katibu wa chama cha walimu Kiteto, Songalael Migire, ameyaeleza hayo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya kiteto akisema kuboreshwa kwa miundombinu ya elimu sambamva na nyumba za waalimu shuleni italeta manufaa katika sekta hiyo

Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Kiteto, Papakinyi Kaai, amekiri Serikali kutambua kazi ya walimu huku Serafine Qoroal Mwanachama wa Chama cha walimu akisisitiza upatijanaji wa viongozi wa Chama hicho kihalali

Suala la waalimu wastaafu kutopatiwa haki zao kwa wakati na hata kurejeshwa kwao wanapostaafu likaibuka, ambapo aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Paulo Gwacha akalitolea ufafanuzi kisha mkuu wa Wilaya ya Kiteto naye akatoa maelekezo ya Serikali

Chanzo: eatv