Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yakifungia kiwanda cha Pombe Kilimajaro

Beer 224651 Serikali yakifungia kiwanda cha Pombe Kilimajaro

Tue, 30 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai amekifungia kiwanda kinachozalisha pombe aina ya simba kutoka kampuni ya Turn Bus Investment, kutokana na kuzalisha pombe zenye kiwango kikubwa cha asidi ambayo sio rafiki kwa afya ya binadamu.

Mbali na kufungia kiwanda hicho ameliagiza Shirika la viwango Tanzania (TBS), mkoani humo kuchunguza viwanda vinavyozalisha pombe zinazotokana na ndizi , ili kujiridhisha kama zinafaa kwa matumizi ya binadamu .

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, amesema amefungia kiwanda kinachozalisha pombe aina ya Simba kilichopo wilayani Rombo kutokana na kuzalisha pombe ambayo haifai kwa matumizi ya binadamu.

Ameongeza kusema kuwa alifika kiwandani hapo na kuchukua sampuli ya pombe na kupeleka TBS na kwamba majibu yametoka kuwa pombe hiyo inayotokana na zao la ndizi haifai kwa matumizi kutokana na kuwepo kwa asidi nyingi.

"Pombe hii aina ya simba inazalishwa kwa wingi wilayani Rombo na kwamba huenda ndio inawaletea madhara vijana wa wilaya hiyo, kwa kuwa kumekuwepo na malalamiko kama inavyo elezwa kuwa vijana wanavimba mashavu pamoja na madhara mengine ikiwemo kutelekeza familia na watoto kutunzwa na bibi wazee."amesema Kagaigai.

Ameongeza kusema kuwa TBS watachukua sampuli ya pombe zinazotokana na ndizi katika viwanda vyote mkoani kilimanjro na kuzichunguza upya ili kuepusha madhara ambayo yanaweza kuwapata vijana ambao ndio wapenzi wa pombe hizo .

Meneja wa viwango TBS kanda ya kaskazini, Happy Kanyeka, amesema katika kiwanda hicho bidhaa ya simba haijakidhi matakwa ya uzalishaji na kwamba kimefungiwa hadi uchunguzi utakapo kamilika.

"Mbali na kiwanda hicho viwanda vyote vinavyozalisha banana Mkoani Kilimanjaro na mikoa mingine vitachukuliwa sampuli upya ili kujiridhisha"

Aidha amesema watafanya uchunguzi zaidi kwa viwanda vya Rombo, kuchunguza malighafi zinazotengeneza pombe hizo na kwamba huenda hawatumii ndizi bali wanatumia malighafi nyingine ambazo zinapeleka kuleta madhara katika pombe hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live