Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yakerwa uzorataji wa mradi wa Sh.bilioni 1 Kilosa

Shemdoe Prof.Riziki Shemdoe, Katibu Mkuu TAMISEMI

Tue, 7 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imeagiza kuharakisha ujenzi wa vituo viwili vya afya vilivyopatiwa fedha mwaka huu 2021/2022 kiasi cha shilingi milioni mia tano pamoja na shule ya sekondari iliyopatiwa shilingi Bilioni moja mara ifikapo mwezi Desemba mwaka huu.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Prof. Riziki Shemdoe, wakati wa ziara yake Wilayani Kilosa.

Prof. Shemdoe amesema kumekuwepo na malumbano ya muda mrefu juu ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa shule ya sekondari iliyotolewa fedha shilingi Bilioni moja kutoka Serikali kuu na vituo viwili vya afya vilivyopatiwa fedha mwaka huu ambapo ujenzi wake bado haujaanza kutokana na sababu zisizo na msingi kama vile mchakato wa manunuzi.

“Nina masikitiko kidogo Kilosa, tumeleta hapa fedha shilingi Bilioni moja kwa ajili ya kujenga shule ya sekondari , mmevutana sana mpaka leo kazi haijaanza, Katibu Tawala Mkoa nakuomba hili ulisimamia kwa karibu mpaka Desemba tuje tuone progress (maendeleo) nzuri shilingi Bilioni moja ipo kwenu imeshindwa kutumika. Tumeleta shilingi milioni mia tano kwa vituo viwili vya afya hilo na lenyewe lianze kufanyiwa kazi” amesema Shemdoe.

Ameongeza kusema kuwa,kero kubwa ambazo walizi wasilisha kwake ya uhaba wa watumishi kama Mhandisi na Mkaguzi wa ndani tayari wameshapelekwa na kwa sasa anaiangalia upya ofisi ya manunuzi kwa kuwa wanaonekana kama wanakwamisha michakato ya manunuzi wilayani humo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live