Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yajenga madarasa 535 Kilimanjaro

Madarasa Ya Mil 520 Yakamilika Njombe, Yakabidhiwa Serikali yajenga madarasa 535 Kilimanjaro

Wed, 22 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amesema katika kipindi cha miaka miwili ya Serikali ya awamu ya sita, mkoa wa Kilimanjaro umejenga vyumba vipya vya madarasa 535 pamoja na shule mpya tisa za sekondari.

Kati ya vyumba hivyo 535 vya madarasa, 401 ni vya shule za sekondari ambavyo ujenzi wake umegharimu zaidi ya shilingi Bilioni nane na kwa upande wa shule za msingi vimejengwa vyumba vipya vya madarasa 134 kwa gharama ya zaidi ya shilingi Bilioni nne.

Aidha shilingi Milioni 831 zimetumika kukarabati madarasa 138 ya shule za msingi mkoani Kilimanjaro na shilingi Milioni 455.5 zimetumika kujenga matundu ya vyoo 414 katika shule za msingi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live