Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yaingilia kati mwili wa mzee uliotelekezwa Shinyanga

91519 Mwili+pic Serikali yaingilia kati mwili wa mzee uliotelekezwa Shinyanga

Mon, 13 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Shinyanga. Serikali ya Tanzania imelazimika kuingilia kati mvutano uliokuwapo kati ya wakazi wa mtaa wa Ngokolo Manispaa  ya Shinyanga na viongozi wao wa mtaa, kugoma kushiriki katika mazishi ya John Tuju (72) kwa kile walichodai jina lake haliko kwenye daftari la mtaa.

Mzee Tuju ambaye alifariki Januari 8, 2020 baada ya kuanguka akiwa barabarani na kupoteza maisha, baada ya taarifa za msiba kutolewa viongozi wa mtaa huo walisema hawamtambui na kuwaeleza wakazi wa mtaa huo ndipo walipoamua kugoma kuzika.

Mzee huyo ambaye alikuwa na ulemavu wa mguu mmoja alikuwa ni maarufu Manispaa ya Shinyanga kutokana na  kuomba omba mitaani ili kujipatia kipato kukidhi mahitaji yake.

Mwenyekiti wa mtaa wa Ngokolo Thomas  Ng’ombe alipoulizwa na waandishi wa habari jana Januari 10,2020 alisema hamtambui mzee huyo kama mkazi wa Ngokolo na kudai  jina lake halimo kwenye daftari la mtaa pia alikuwa hahudhurii kwenye misiba.

"Jana ndiyo tulipata taarifa za msiba na kuanza kufuatilia ili kuona jinsi ya kusaidia mazishi, lakini pia mtaa (nzengo) wetu hatumtambui kama mkazi waeneo hili,” amesema mwenyekiti wa mtaa.

Kutokana na mvutano huo ofisa mtendaji wa kata ya Ngokolo, Felister Msemelwa aliuagiza uongozi wa serikali ya mtaa huo kumzika mzee huyo kwa kufuata taratibu zote na heshima kama wanavyofanya mazishi ya watu wengine.

Chanzo: mwananchi.co.tz