Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yafuta umiliki wa mashamba matatu Tanga

73630 Shamba+pic

Fri, 30 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tanga. Serikali Agosti 30 2019 imefuta miliki ya Mashamba matatu ya Mkomazi Plantantions maarufu MOA yaliyopo wilaya ya Mkinga mkoani Tanga kutokana na kukiuka masharti ya uendelezaji ikiwemo kutelekezwa bila kufanyiwa maendelezo yaliyokusudiwa na kutolipiwa kodi ya pango la ardhi.

Uamuzi huo umetangazwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alipozungumza na wananchi wa Mayomboni wilayani Mkinga alipokwenda kutatua mgogoro wa muda mrefu katika eneo hilo.

Alisema uamuzi wa kufuta mashamba hayo matatu unafuatia maombi yaliyotumwa kwa Raisi John Magufuli ya kutaka kufutwa mashamba hayo kutokana na kutoendelezwa na wamiliki wake kwa muda mrefu.

Alisema Rais ameridhia maombi hayo kwa kuwa serikali imekuwa ikisisitiza utekelezwaji wa sheria ya Ardhi Na 4 ya 1999 ikiwemo uendelezaji wa mashamba ambayo yamemilikishwa sehemu mbalimbali nchini.

Ameagiza kufanyika upimaji katika vijiji vyote kumi vilivyopo ndani ya shamba hilo sambamba na kuanishwa miapaka ya vijiji hivyo na kupatiwa hati ambapo alitaka wananchi wanaishi kwenye vijiji hivyo kutobughudhiwa.

Mashamba yaliyofutiwa ni lenye hati Na. 9780  na ukubwa wa ekari 14,688, shamba  Na. 4268  ekari 804 na shamba lenye hati Na. 9781  ekari 246 ambapo mashamba yote matatu yana ukubwa wa ekari 15,738.

Pia Soma

Advertisement   ?
Kufuatia uamuzi huo, jumla ya vijiji 10 vyenye kaya 3,236 zilizo na wakazi 16,450 zitanufaika na uamuzi wa Serikali kutokana na wananchi wake kufanya maendelezo ya kujenga makazi, shule pamoja na kuendesha shughuli za kilimo cha mazao ya kudumu na ya muda mfupi.

Vijiji vilivyonufaika ni uamuzi wa Serikali kufuta mashamba ya Mkomazi Plantations ni kijiji cha Kilulu-Dunga, Zingibari, Mwaboza, Mwakikoya, Mhandakini, Nkanyeni, Sigaya, Mayomboni, Ndumbani pamona na kijiji cha Moa

Katika hatua nyingine Waziri Lukuvi ameagiza kufanyika uhakiki wa mashamba mengine ya Kwa Mtili Estates Co Ltd yaliyopo mkoani humo ambapo ekari 58 pekee ndizo zilizoombwa kufutwa kwa Rais kutokana na kutoendelezwa huku mmili wake ikidaiwa kumiliki ekari  2,841.

Hatua hiyo inafuatia Mkuu wa Idara ya Ardhi na Maliasili katika halmashauri ya wilaya ya Mkinga Obed Katonge kueleza kuwa Kwa Mtili Estates Co Ltd inalo shamba la lenye ukubwa wa ekari 2,841 tofauti na inavyoonekana katika kumbukumbu za ofisi ya Msajili wa Hati Kanda ya Kaskazini ambazo ni 58.

Mbunge wa Jimbo la Mkinga mkoani Tanga Dustan Kitandula ameishukuru Serikali kwa kusikiliza kilio cha muda mrefu cha wananchi wanaoishi eneo la shamba lililofutwa la kutaka kurejeshewa ardhi yao waliyokuwa wakiutumia kwa shughuli mbalimbali.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz