Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yafanya msako kuwasaka watoto amabo hawajaripoti shule

Utata Shule Mkuu.png Serikali yafanya msako kuwasaka watoto amabo hawajaripoti shule

Wed, 17 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

iku chache baada ya JamiiForums kuripoti juu ya Shule ya Msingi ya Mlembea Wilayani Rombo kuandikisha Wanafunzi Watatu pekee wa Darasa la Kwanza, baadhi ya Wananchi wamedai moja ya changamoto inayosababisha hali hiyo ni uongozi wa Shule.

Mwananchi mmoja amesema “Watoto wangu wawili wamesoma hapo, nimelipa hela ya chakula lakini unakuta wanakula miezi miwili tu, pia kuna matumizi mabaya ya fedha lakini kwa Mwaka huu hakuna Watoto wengi wameenda sehemu nyingine kusoma.”

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Raymond Stephen Mwangwala amesema “Tunatoa wito kwa Wazazi na walezi ambao hawajaleta Watoto shuleni wana siku chache za kufanya hivyo.

“Kwa sasa kazi inayoendelea ni viongozi wa Serikali kuanzia ngazi ya Vitongoji, Tarafa, Kata, Waratibu wa Elimu na Maafisa Tarafa kuhakikisha wanatembea vitongoji vyote kuhakikisha Watoto wote wanaostahili wanapelekwa shule.

“Endapo kutakuwa na yeyote anayezuia Mtoto kwenda shule kwa makusudi atambue kuwa kusoma ni haki ya msingi ya Mtoto.

“Nitoe wito kwa Wazazi na viongozi, yeyote atakayeona mtoto anazagaa mtaani wakati wa shule atoe taarifa kwa mamlaka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live