Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yaanza mkakati wa kunusuru watu kuliwa mamba Ziwa Victoria

Ziwa Victoria Mambaaa Serikali yaanza mkakati wa kunusuru watu kuliwa mamba Ziwa Victoria

Fri, 17 Mar 2023 Chanzo: mwanachidigital

utokana na watu kupoteza maisha kwa kushambuliwa na mamba na wengine, kutapa ulemavu wa kudumu wakati wanafanya shughuli mbalimbali ndani ya Ziwa Victoria, Serikali imeanza mkakati wa kujenga vizimba ndani ya Ziwa Victoria ambavyo wananchi watavitumia kwa ajili ya shughuli za kibinadamu.

Vizimba hivyo vinajengwa mwalo wa Kijiji cha Kanyala, Kata ya Bulyaheke sambamba na Kijiji cha Izindabo, Kata ya Nyakasasa kisiwani Kome, Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza.

Mradi huo wa vizimba unatekelezwa na Wizara ya Maliasili na Utalii utasaidia wananchi wa maeneo hayo ambao walikuwa wanapoteza maisha kwa kushambuliwa na mamba na wengine kupata ulemavu wa kudumu.

Ofisa wanyamapori msaidizi kutoka Taasisi ya Utafiti Wanyamapori (Tawiri) iliyo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Mohamed Mpoto amesema licha ya mkakati wa kujenga vizimba wametoa elimu mbalimbali kwa wananchi namna ya kuepuka kushambuliwa na mamba Ziwa Victoria wakati wanafanya shughuli mbalimbali.

Hata hivyo, amesema taasisi ya wanyamapori imekuwa ikitoa kifuta machozi kwa watu waliopoteza maisha na wengine waliopata ulemavu wa kudumu kwa kushambuliwa sambamba na watu mazao yao yaliyoharibiwa na wanyama wakali hasa viboko.

Mpoto amesema mwaka 2021/2022 serikali imetoa Sh13.4 milioni za kutoa kifuta machozi kwa watu 61 kati hao watu watano waliokufa kwa kushambuliwa namba wawili waliopata ulemavu wa kudumu na watu 54 ambao mazao yao yalihabiwa na wanyama wakali hususani viboko na fedha hizi zinatolewa na taasisi ya wanyamapori Tanzania.

Kwa mwaka 2023 kuanzia mwezi Januari watu saba wamepoteza maisha kwa kushambuliwa na mamba akiwa mama mmoja Editha Ndakadi aliyeacha watoto sita yatima kwenye Kitongoji cha Bwego Kijiji cha Kanoni, Kata ya Maisome Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza baada ya kushambuliwa na mamba.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Buchosa Wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza, Mwita Waryoba amesema wamepokea ushauri wa wananchi juu ya kuajiri Idara ya wanyamapori ili kuwasaidia wananchi.

Kwa mwaka 2023 maombi ya watu 77 wa kisiwa cha Maisome ambao mazao yao yameharibiwa na wanyama na wakali na wengine kupoteza maisha huku wengine wakipata ulemavu wa kudumu yametumwa taasisi ya wanyamapori kwa ajili ya kuandaliwa malipo ya kifuta machozi.

Elimu na njia ya kuepuka kushambuliwa na mamba inayotolewa na taasisi ya wanyamapori ni kuepuka kufua, kuchota maji maeneo ya ya mto au ziwa yasiyokuwa na vizimba sambamba na maeneo yenye nyasi nyingi na vichaka, kuepuka kuvua samaki kwa maeneo ya mapango.

Pia njia ya kujiokoa wakati wa kushambuliwa na mamba ni kutumia vidole, kifaa chenye ncha kali kumchoma mamba machoni kutokana na udhaifu wa mamba anapokuguswa kwenye macho huwa hana ujanja wowote.

Changamoto ya taarifa

Changamoto inayowakabili watu waliopoteza maisha kwa kuliwa na mamba huku wengine kupata ulemavu wa kudumu kuzifikia mamlaka husika ili wapate kifuta machozi.

Taasisi ya Tawiri inaziomba halmashauri kuajiri maofisa wanyamapori watakaosaidia kutoa taarifa na kuacha kuwatumia watendaji wa kata na vijiji.

Wasemavyo wananchi

Wananchi wameiomba vizimba viongozeke maeneo mbalimbali kutoka na uhitaji wa wananchi ili kuepuka kuliwa na mamba.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Kanyala, Gacha Paul amesema serikali imefanya jambo jema kuwasaidia wananchi wake hii itakuwa ndiyo njia pekee ya kuwanusuru kuliwa mamba.

Mmoja wa wananchi wa Kata ya Bulyaheke, Amina John amesema kuna tatizo la matukio mengi hayaripoti ya watu waliopoteza maisha kwa kuliwa na mamba, hivyo serikali kupima halmashauri husika waajiri maofisa ambao watahusika na jambo hilo ili wananchi waweze kusaidiwa.

Chanzo: mwanachidigital