Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yaanza kukarabati miundombinu Kilosa

Kilosa Mhm.jpeg Serikali yaanza kukarabati miundombinu Kilosa

Sun, 10 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Dar es Salaam. Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, mkoani Morogoro, Shaka Hamdu Shaka amesema wameanza kurekebisha miundombinu iliyoharibiwa na mvua kubwa iliyonyesha jana Jumamosi.

Shaka amesema mvua hiyo iliyoambatana na maji mengi yaliyokuwa yakitirika kutoka milimani, yaliyosababisha kuvunjika kwa madaraja matatu na kukata mawasiliano kutoka upande mmoja kwenda mwingine.

Hii ni mara pili mvua hizo kuleta madhara wilayani humo, kwani mara ya kwanza Desemba 5 mtu mmoja mwanaume alifariki dunia wakati akijaribu kujiokoa baada ya maji kuingia katika nyumba yake usiku kufuatia mvua kubwa ilinyesha maeneo ya Rudewa na Mvumi.

Akizungumza na Mwananchi leo, Jumapili Desemba 10, 2023 Shaka amesema mvua hizo hazijaleta madhara kwa binadamu pekee, bali imeahiribu miundombinu ikiwemo madaraja na makazi ambayo bado idadi yake haijajulikana.

“Taasisi za Serikali ikiwemo Tarura (Wakala wa Barabara za Mijini na Vijini), Tanroads (Wakala wa Barabara Tanzania) zipo kazini kurebisha uharibifu uliotokea. Kuna daraja la Mto Mkondoa, Mazinyungu na Ilonga yote yamesombwa na maji.

“Hadi jana usiku mawasiliano yalikatika tulikuwa Kilosa hatuwezi kwenda ng’ambo ya pili na wale wa upande wa pili hawawezi kuja Kilosa, ila tumejitahidi sasa watu wanapita njia za mchepuko,” amesema Shaka.

Shaka amesema si taasisi hizo peklee, bali hadi mamlaka myingine zikiwemo za kamati ya ulinzi na usalama zote zipo kazini kuhakikisha hali inakuwa ya kawaida kwa maeneo yaliyoathiriwa na mvua hizo.

“Bado hatujafanya tathimini ya kubaini makazi yaliyoathirika na mvua hizi. Mvua ilinyesha, lakini kuna maji mengi yalitiririka kutoka mlimani kuanzia saa moja usiku hadi saa nane usiku,”amesema Shaka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live