Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yaanza kufunga kamera kwenye magereza

Serikali Yaanza Ufungaji Wa  Kamera Magerezani Serikali yaanza kufunga kamera kwenye magereza

Sun, 14 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imeanza Ufungaji wa Kamera maalumu(CCTV) katika maeneo mbalimbali yanayozunguka magereza lengo ikiwa ni Uboreshaji wa Huduma za ulinzi na usalama pamoja na kwenda na dhana nzima ya sayansi na teknolojia katika utoaji na ufuatiliaji wa huduma kwa wadau mbalimbali wanaoshilikiana na Jeshi la Magereza ikiwemo Jeshi la Polisi na Mahakama.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Kamishna wa Jeshi la Magereza, Jeremia Katungu wakati akizungumza mbele ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Daniel Sillo wakati wa mkutano uliohusisha Uongozi wa juu wa jeshi hilo, Maafisa, Askari na watumishi raia huku akitaja baadhi ya mikoa ambapo kamera hizo zimefungwa.

"Tunaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuliwezesha jeshi katika maeneo mbalimbali ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake, baadhi ya maeneo hayo ni ununuzi wa vifaa vya ulinzi na usalama katika maeneo yanayozunguka magereza kwa nje ambapo kwa sasa zoezi la usimikaji wa vifaa hivyo kwa sasa unaendelea katika maeneo ya magereza ya Maweni, Karanga, Moshi, Lwanda na Tabora." amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live