Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yaahidi umeme Tabora nzima

Umeme Tanesco Wilaya zote Tabora kufikiwa na huduma ya Nishati ya umeme

Wed, 18 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imeweka mkakati wa kuhakikisha inaunganisha wilaya zote za Tabora kuwa na umeme wa uhakika.

Hayo yamesemwa leo Mei 18, 2022 na Waziri wa Nishati, Januari Makamba katika ufunguzi wa barabara ya Tabora, Koga – Mpanda KM 342.9.

Amesema Mkoa wa Tabora unategemea umeme kutoka kituo cha Kaloleni kilichopo Tabora mjini na kiutaalamu waya wa kilovolti 33 unapaswa kusafirisha umeme kwa kilometa 100.

“Lakini hapa unasafirisha kwa kilometa 1,200, kwa hiyo umeme kwa maeneo mengi unafika ukiwa hauna nguvu, ”amesema Makamba.

Amesema kwa upande wa Wilaya ya Sikonge, kuna suala la uhakika wa upatikanaji wa umeme yaani umeme kufika bila kukatikakatika, imekuwa ni changamoto ya muda mrefu, lakini wameshughulikia na kupunguza urefu wa waya unaoleta umeme katika wilaya zote za Mkoa wa Tabora

“Kazi ambayo tumeifanya kwa kipindi cha miezi sita ni kupunguza urefu wa waya unaopeleka umeme maeneo mbalimbali, tumeanza na Kaliua na Sikonge, kwa hiyo wilaya hizo zitapata umeme kwa uhakika zaidi. Kazi nyingine zinaendelea katika wilaya zingine,” amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live