Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yaahidi kutoa bilioni 2 maboresho DMI

Maritime Pic Databb Serikali yaahidi bilioni 2 maboresho DMI

Thu, 7 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imeahidi kutoa jumla ya shilingi bilioni 2 kwa ajili ya kuboresha miundombinu kwenye Taasisi ya elimu ya usafiri wa majini DMI, ili kuweza kutoa elimu inayokidhi viwango vinavyohitajika kimataifa.

Haya yamebainishwa na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara wakati alipo tembelea Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa kila siku teknolojia duniani inakua, hivyo vifaa kazi vinavyotumika kufundishia vinapaswa viwe vya kisasa ili kuweza kupata wajuzi waliobobea, sambamba na hilo ameongeza kusema kuwa majengo katika Taasisi hiyo hayasanifu aina ya elimu inayotolewa.

"Ili kuweza kuhakikisha kuwa chuo hiki kinapata hadhi ya kimataifa, inabidi kufanya maboresho makubwa" amesema Waitara.

Mbali na hayo, Waitara amesema kuwa bado Serikali itaendelea kutenga bajeti ya kutosha kwa ajili ya kufanya maboresho kwa vyuo vyote vya Serikali nchini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live