Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali ya Tanzania yasaini mkataba ujenzi barabara ya lami Tanga - Pangani

69229 BARABARA+PIC

Thu, 1 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Pangani. Mkataba wa ujenzi wa barabara ya Tanga - Pangani nchini Tanzania yenye urefu wa kilomita 50 kwa kiwango cha lami, umesainiwa rasmi jana Jumatano Agosti 31, 2019.

Kujengwa kwa barabara hiyo kunawapatia matumaini wakazi wa wilaya hiyo walioisubiri kwa miaka 58.

Licha ya kwamba Pangani ni Wilaya Kongwe iliyokuwapo tangu enzi ya utawala wa Kijerumani, lakini miundombinu yake ya barabara mibovu hali inayosababisha kero kubwa kwa wananchi wanaotumia.

Mkataba wa ujenzi wa barabara hiyo ulisainiwa jana mbele ya mkutano wa hadhara baina ya Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (Tanroads), Partick Mfugale na mwakilishi wa kampuni iliyopewa zabuni ya kujenga barabara hiyo ya China Henan Internatinal Company Limited (Chico) kutoka China.

Akizungumza baada ya kusaini makataba huo ambao pia ulishuhudiwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe, wajumbe wa kamati ya

Bunge ya Miundombinu, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela na Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Awesso, Mfugale alisema ujenzi wake utagharimu Sh66.8.bilioni.

Pia Soma

“Tutahakikisha tunamsimamia mkandarasi huyu aweze kumaliza barabara hii kwa muda,” alisema Mfugale.

Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri Kamwelwe alisema barabara hiyo ni miongoni mwa zinazopita kando ya Bahari ya Hindi ya Afrika Mashariki kutoka Lamu-Lungalunga – Horohoro – Tanga – Pangani - Saadani hadi Bagamoyo ikiwa na urefu wa kilomita 454.

“Kutokana na gharama za ujenzi wa madaraja ya mito ya Pangani na Wami, wafadhili wa mradi walikuwa wakisita, hivyo Serikali ikaamua kutoa fedha zake kuijenga hii ya Tanga - Bagamoyo” alisema Kamwelwe.

Waziri huyo alisema hata hivyo, Rais John Magufuli alisema tayari Serikali imepata Sh350 bilioni zitakazojenga Daraja la mto Pangani na kilomita 120 za barabara ya kutoka Pangani - Sadani hadi Mkurunge.

“Hivi karibuni mtashuhudia tena tukio la kusaini mkataba wa ujenzi wa daraja la Mto Pangani na kipande cha Pangani - Sadani hadi Mkurunge,” alisema Kamwelwe.

Mbunge wa Pangani, Jumaa Aweso aliishukuru Serikali kwa kuijenga barabara hiyo kwa sababu licha kuwa ni kero ya muda mrefu, lakini pia ni ahadi aliyotoa Rais Magufuli wakati akiomba kura za kupewa ridhaa ya kuwa Rais.

Mkazi wa Pangani Mashariki, Fatma Mtungakoa alisema tukio la kujenga hiyo litakuwa limemaliza kiu ya wakazi wa wilaya hiyo ambao wamekuwa wakiahidiwa kwa kipindi kirefu.

Chanzo: mwananchi.co.tz