Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali ya Tanzania: Hakuna ushahidi wa umbali husababisha mimba shuleni

Thu, 20 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Serikali ya Tanzania imesema hakuna tafiti maalumu zinazothibitisha umbali wa kwenda shule ni chanzo cha mimba za wanafunzi.

Kauli hiyo imetolewa leo Alhamisi bungeni Juni 20, 2019 na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi, Josephat Kandenge wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Rombo (Chadema) Joseph Selasini ambaye ameuliza ni lini Serikali itamaliza kero za wanafunzi wa kike kwa kujenga mabweni ili kupunguza mimba mashuleni.

Katika swali la msingi, mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Anna Gidarya ameuliza Serikali ina mkakati gani wa kujenga bweni kwa kila shule ya kata ili kuondoa kero ya kutembelea umbali mrefu na kuondoa mazingira yasiyo rafiki kwa wanafunzi wa kike waliopanga mtaani.

Naibu Waziri amesema shule za kata zilisajiliwa kama shule za kutwa lakini Serikali imeliona juu ya wanaotembea muda mrefu na kwa kushirikiana na wadau wengine, wameanza ujenzi wa hosteli.

Ametolea mfano katika mwaka wa fedha wa 2018/19, Serikali kupitia mradi wa lipa kulingana na matokeo EP4R ilijenga vyumba vya madarasa 938, matundu ya vyoo 2,141,mabweni 210,nyumba za walimu 47,maabara 22,maktaba 39 na mabwalo ya chakula 76.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz