Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kutoa viwanja 10,000 wanaohama Ngorongoro

Msomera Wamasai Kuhama (600 X 456) Serikali kutoa viwanja 10,000 wanaohama Ngorongoro

Fri, 8 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jumla ya viwanja 10,000 vinatarajiwa kupimwa katika sehemu ya eneo lililokuwa Pori Tengefu la Handeni awamu ya pili kwa ajili ya wakazi wanaohama kwa hiari kutoka hifadhi ya Ngorongoro.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Geophrey Pinda akiwa katika eneo linalotekelezwa mradi wa kupima viwanja na mashamba wakati wa ziara ya pamoja baina yake na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye kijiji cha Msomera, Handeni, Mkoa wa Tanga.

Pinda amesema kati ya viwanja hivyo, viwanja 5,000 ni kwa ajili ya makazi na 5,000 ni mashamba. Kwa mujibu wa Naibu Waziri huyo viwanja 2,500 vya makazi vitapimwa kwenye kijiji cha Msomera, viwanja 1,500 katika kijiji cha Kitwai B (Simanjiro) na viwanja 1,000 kijiji cha Sauyi (Kilindi).

Aidha, amesema hadi kufikia Februari 28 mwaka huu, jumla ya viwanja 5,882 vilikuwa vimepimwa, sawa na asilimia 118 ya lengo la kupima viwanja 5,000 katika vijiji vya Saunyi (Kilindi) na Msomera (Handeni).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live