Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kutoa vishikwambi kupata taarifa za Ebola

Bukoba Pic Data Serikali kutoa vishikwambi kupata taarifa za Ebola

Tue, 4 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wahudumu wa afya ngazi ya jamii mkoani Kagera wapatao 90 wanatarajiwa kupatiwa vishikwambi kwa ajili ya kutoa taarifa za tetesi kuhusu wahisiwa wa ugonjwa wa Ebola ambazo watakuwa wanazipata kutoka katika jamii yao.

Hayo yameelezwa leo Oktoba 3 na Mkurugenzi wa Idara ya Kinga kutoka Wizara ya Afya, Dk Beatrice Mutayoba alipokuwa akizindua mafunzo ya siku mbili yanayofanyika Manispaa ya Bukoba kwa timu za uendeshaji wa huduma za afya ngazi ya mkoa na timu za uendeshaji wa huduma za afya ngazi ya halmashauri (CHMT’S).

Amesema kuwa, baada ya timu hizo kupata elimu watakwenda kuwaelimisha watoa huduma ngazi ya jamii ambao baada ya mafunzo watapatiwa vishikwambi.

“Tunatarajia kutoa vishikwambi 90 kwa watoa huduma ngazi ya jamii ambavyo vitasaidia katika utoaji wa taarifa za tetesi kwa wahisiwa wa ugonjwa wa Ebola na watoa huduma hao watatoa taarifa hizo kwa watoa huduma ngazi ya wilaya ili tetesi hizo zifanyiwe kazi haraka,” amesema Dk Mutayoba.

Naye Mganga Mkuu wa Wilaya ya Misenyi, Daniel Chochole ambaye wilaya yake inapakana kabisa na nchi ya Uganda ameendelea kuhamasisha jamii ya wilaya hiyo kuwa waendeleze utamaduni wa kunawa mikono mara kwa mara na maji safi tiririka yenye sabuni kwa ajili ya kujikinga na magonjwa.

Aidha amehamasisha wananchi hao kutoa taarifa popote watakapomuona muhisiwa mwenye dalili za ebola ambazo ni kutapika, kutoa damu sehemu mbalimbali za viungo vya mwili, homa ya ghafra na wasimguse mtu wa namna hiyo.

Alinda Rwezaula mkazi wa Manispaa ya Bukoba amesema kupitia njia mbalimbali zikiwemo za vyombo vya habari wanaendelea kupata elimu juu ya kujinga na ebola na wamejifunza iwapo atapatikana mmtu mwenye dalili kwenye maeneo yao watoe taarifa haraka ili mtu huyo aweze kupimwa na atakapobainika aanze matibabu katika vituo maalum vya tiba.

Tayari Mkoa wa Kagera tayari umepata maabara tembezi ya kupima virus vya ebola na Mashine yenye zaidi ya Sh600 milioni imefungwa kituo cha afya Kabyaire kilichopo Wilaya ya Misenyi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live