Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kutatua kero ya maji Kiteto

Maji Dar Balaa Serikali kutatua kero ya maji Kiteto

Tue, 15 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali wilayani Kiteto mkoani Manyara, imesikia kilio cha wananchi wa eneo la Lugejuu Kata ya Partimbo, ambao kwa sasa wanatumia maji  yasio safi na salama wanayotumia na wanyama, kwa kuanzisha mradi wa maji unaogharimu Sh. mil 453 utakaoondoa adha hiyo.

Mradi huo wa maji uliopo Kata ya Kibaya ambao tanki lake limejengwa eneo la Kigamboni Kata ya Partimbo utakuwa suluhisho la tatizo la maji mjini Kibaya, tatizo lililokudumu kwa muda mrefu uliopelekea kuvunja ndoa za watu kwa kutumia muda mrefu kutafuta maji.

Katika Kikao kilichoketi chini ya Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mbaraka Batenga pamoja na mambo mengine tatizo la maji likazungumzwa huku mkuu wa Wilaya akionya ubadhirifu wa fedha katika mradi huo huku wananchi wakishukuru serikali kwa utatuzi wa changamoto hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live