Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kupima eneo la KIA kumaliza mgogoro

Serikali Pic KIA KIA Serikali kupima eneo la KIA kumaliza mgogoro

Thu, 3 Nov 2022 Chanzo: mwanachidigital

Serikali imesema itapima eneo lote la uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na Kampuni ya uendeshaji ya Uwanja huo (KADCO), ili kumaliza mgogoro uliodumu kwa zaidi ya miaka 20 kati ya kampuni hiyo na wananchi wanaouzunguka.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Kia, wilayani Hai.

Babu aliyeambatana na Kamati ya Usalama ya Mkoa huo amesema Serikali kwa kushirikiana na jopo la wataalam watapima eneo lote la KIA Novemba 11 mwaka huu na kujua ni nani yupo ndani au nje ya eneo la uwanja huo.

"Haya ni maelekezo ya serikali kwamba Novemba 11 tutaanza kupima maeneo yote na mtu atakayebainika hakuingia ndani ya uwanja wa KIA hatutamgusa na wala hatutakuwa na shughuli naye, lakini walioingia ndani ya uwanja wataondoka na tutawalipa ili ahamie eneo," amesema RC Babu.

Babu amesema lengo la kupima maeneo hayo ni kujua ni nani ameingia ndani ya uwanja wa ndege wa KIA na nani yupo nje ya uwanja huo, ambapo watathmini wataweka alama kwenye maeneo yote ya uwanja wa KIA.

"Tunachowaambia leo ni maagizo ya Serikali kwamba tunafanya kazi ya kupima eneo lote la uwanja wa ndege wa KIA alafu tujue nani yupo ndani ya eneo la uwanja na ni yupo nje ya uwanja ambao wapo ndani ya uwanja wataondoka na tuawalipa haki zao," amesema RC Babu

Awali diwani wa kata hiyo, Tehera Mollel amesema mgogoro huo umeanza kwa muda mrefu bila kupatiwa ufumbuzi na kuiomba serikali kutoa tamko rasmi la suluhisho la mgogoro huo.

"Mgogoro wetu na KADCO umedumu kwa miaka mingi lakini leo naomba utupe majibu sahihi ya nini tamko la Serikali kuhusu mgogoro huu sugu ambao unaumiza wananchi wa kata yangu ya KIA," amesema Mollel.

Akisoma taarifa ya mgogoro huo, mmoja wa wananchi wa kata ya Kia, Stephen Laizer amesema mgogoro huo umeanza muda mrefu ambapo eneo linalosababisha mgogoro huo ni eneo lenye ukubwa wa zaidi ya hekta 11,000.

"Tunaomba iundwe tume huru kuchunguza mgogoru huu ili uweze kutoa maamuzi ya haki kwa vijiji vinavyozunguka uwanja wa ndege wa KIA," amesema.

Chanzo: mwanachidigital