Serikali ina mpango wa kuanza ujenzi wa barabara za mabasi yaendayo haraka 'mwendokasi' inayotoka Kigogo - Tabata Dampo hadi Segerea mkoani Dar es Salaam ili kuendelea kurahisisha huduma za usafiri kwa wakazi wa mkoa huo.
Serikali ina mpango wa kuanza ujenzi wa barabara za mabasi yaendayo haraka 'mwendokasi' inayotoka Kigogo - Tabata Dampo hadi Segerea mkoani Dar es Salaam ili kuendelea kurahisisha huduma za usafiri kwa wakazi wa mkoa huo. Akijibu swali bungeni jijini Dodoma, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt. Festo Dugange amesema barabara ya mwendokasi ya Kigogo - Tabata Dampo hadi Segerea ni miongoni mwa barabara ambazo zimepangwa kujengwa katika awamu ya tano ya ujenzi wa miundombinu ya mabasi hayo yaendayo haraka.