Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kumaliza kero ya umeme Kigoma 2022

Kigoma Kigoma 1.jfif Waziri wa Nishati, Januari Makamba akikagua mradi wa umeme Kigoma

Wed, 6 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Nishati, Januari Makamba tayari amewasili Mkoani Kigoma kwa ajili ya kutekeleza maagizo ya Makamu wa Rais Dkt. Philips Mpango, aliyoyatoa kwa Wizara hiyo kuitaka imalize tatizo la umeme Mkoani hapo.

Waziri Makamba amesema ifikapo tarehe 25 mwezi Novemba 2021, Wizara hiyo kupitia Shirika la umeme nchini Tanesco, litakuwa limemaliza tatizo la umeme ambalo limekuwa kikwazo kikubwa kwa wananchi mkoani hapo .

Amesema kuwa Mkoa huo upo nje ya Gridi ya Taifa ya umeme jambo ambalo linapelekea Tanesco kutumia zaidi ya bilioni 3 kwa mwezi kununua mafuta ya dizeli yanayotumika kutoa huduma ya umeme kwa jamii.

Aidha ameahidi kuleta Gridi ifikapo mwaka 2022 kwani manunuzi hayo ya sasa ni kwa wateja wapatao 63,000 wanaolipa zaidi ya bilioni 1.5.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live