Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kujenga mradi wa maji Chamwino

2de61e0fc4ff2b4ef4f2b398359bde0a Serikali kujenga mradi wa maji Chamwino

Sat, 6 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Mbunge wa Chamwino Jijini Dodoma, Deo Dejembi amesema kuwa Serikali ipo katika mpango wa kujenga mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya Shilingi milioni 500 katika katika Kata ya Dabalo wilayani Chamwino.

Dejembi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma amebainisha hayo leo jimboni humo alipokuwa ziarani kutembelea wapiga kura wake.

“Serikali ndani ya miezi mitatu baada ya kufuatilia imekubali kuleta mradi mkubwa wa maji hapa Dabalo ili kumtua Mama Ndoo na utakuwa msaada pia kwa maeneo jirani ya Segala na Membe” amesema Dejembi.

Chanzo: www.habarileo.co.tz