Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kujenga daraja Songea-Nyasa

BASHUNGWAAA Serikali kujenga daraja Songea-Nyasa

Tue, 16 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema serikali ipo mbioni kujenga daraja la kisasa kwenye Mto Mitomoni, Kijiji cha Mapotopoto ambalo litaunganisha Wilaya ya Songea Vijijini na Nyasa mkoani Ruvuma.

Hayo ameyasema leo Aprili 16,2024 wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Jackiline Ngonyani bungeni Dodoma.

“Maandalizi ya nyaraka kwa ajili ya kutangaza zabuni kwa mara ya pili kwa ajili ya ujenzi wa daraja la mitomoni yapo katika hatua za mwisho na zabuni zinatarajiwa kutangazwa kabla ya mwisho wa mwezi Juni wa mwaka huu 2024,” amesema Waziri Bashungwa.

Aidha, amesema zabuni za mara ya kwanza zilikamilika Machi 2023 zilikosa ushindani kwani Mkandarasi mmoja tu ndiye aliyerudisha zabuni na bei yake ilikuwa juu hivyo wakaona watangaze upya.

Vilevile, Waziri Bashungwa, amesema Serikali ipo pamoja na Wananchi wa Wilaya ya Nyasa pamoja na Songea Vijijini, na ndio maana wanafanya juhudi ili kuweza kukamilisha manunuzi ili kumpata mkandarasi wa kujenga daraja la kudumu.

Pia, Bashungwa amemhakikishia mbunge huyo kuwa kufika mwezi wa sita hatua za manunuzi zitakuwa zimekamilika ili hatua za ujenzi wa daraja hilo ziweze kuanza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live