Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kufunga kamera za usalama Dodoma

28612828214e0a0a6644d48a3ca5be98.jpeg Serikali kufunga kamera za usalama Dodoma

Sun, 20 Jun 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

SERIKALI imedhamiria kufunga kamera za usalama katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dodoma kwa lengo la kupunguza uhalifu ambao umeanza kujitokeza katika maeneo mbalimbali baada ya Serikali kuhamia huko.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka alisema hayo jana wakati wa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Kituo cha Polisi Chang’ombe, jijini Dodoma.

Ujenzi wa kituo huo umechochewa na kukithiri kwa vitendo vya uhalifu ikiwemo uporaji, ubakaji, udhalilishaji, matumizi ya dawa za kulevya katika maeneo ya Chang’ombe hali inayosababisha wananchi wa maeneo hayo kuishi kwa wasiwasi.

“Maeneo mengi ya jiji la Dodoma tutafunga kamera za usalama barabarani, hatuwezi kuwa na jiji ambalo polisi wetu wanakimbizana na wahalifu muda wote, tutatumia teknolojia hiyo

kudhibiti uhalifu wa aina mbalimbali, Dodoma ni Makao Makuu ya nchi lazima pawe salama nawashauri wahalifu watafute shughuli nyingine ya kufanya hapa si salama tena kwa kazi zao,” alisema Mtaka

Akizungumzia ujenzi wa kituo hicho cha Polisi, Mtaka aliwataka wananchi kushirikiana na serikali kuhakikisha ujenzi wake unakamilika mapema kianze kutoa huduma za kiusalama katika maeneo hayo.

“Chang’ombe inakua inahitaji kituo kikubwa kita-

kachofanya kazi saa ishirini na nne ili wafanyabiashara na wananchi wafanye shughuli zao kwa muda wote na sio biashara zifungwe kwa kuhofia uhalifu, sasa kazi ya serikali sio kukwambia ufunge biashara yako muda gani kazi ya serikali ni kukulinda ili kuwepo na uhuru wa kutoa huduma, kwahiyo wananchi tushirikiane ili kituo kimalizike haraka” alisema Mtaka Akizungumza kwa niaba ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Naibu Katibu Mkuu, Ramadhani Kailima

alisema wizara imetoa Sh milioni 10 kama mchango wake katika ujenzi wa kituo hicho na kikikamilika kitatoa huduma mbalimbali ikiwemo upelelezi wa matukio, upelekaji wa majarlada ya kesi kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mashitaka ambayo yatapelekwa mahakamani kwa hatua za kisheria.

Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde alichangia papo hapo mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho na alimkabidhi Mkuu wa Mkoa, Mtaka.

Chanzo: www.habarileo.co.tz