Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kuangalia fursa za kiuchumi ujenzi wa reli Tunduma

48b39cce60a0da205bdf7720fd1a6c7a Serikali kuangalia fursa za kiuchumi ujenzi wa reli Tunduma

Wed, 31 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya amesema ujenzi wa reli kutoka Tunduma hadi Kasanga utazingatia matokeo ya upembuzi yakinifu utakaofanywa na Serikali kubaini utafungua vipi fursa za kiuchumi katika maeneo hayo.

Kasekenya amebainisha hayo leo bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Kalambo, Josephat Kandege lililohoji kwanini Serikali haioni umuhimu wa kujenga kipande hicho cha reli kitakachosaidia matumizi mazuri ya Bandari ya Kasanga kitu kitakachopelekea Mkoa wa Rukwa kufunguka kiuchumi.

“Naomba kumhakikishia mheshimiwa mbunge kuwa ushauri wake tumeupokea na tutaufanyia kazi kwakuwa utekelezaji wa miradi ya reli inahitaji fedha nyingi hivyo ushauri huu utazingatia matokeo ya upembuzi yakinifu kuhusu kipande hicho kwa kuangalia ni vipaumbele vipi ambavyo nchi imeviweka” amesema Kasekenya.

Aidha, Kasekenya amesema kuwa kipindi cha ukoloni ilifanyika tathimini kwa ajili ya ujenzi wa kipande hicho hivyo wana mpango wa kuipitia upya kwakuwa kwa sasa mazingira yamebadilika.

Chanzo: www.habarileo.co.tz