Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali imetoa bilioni 1.2 kusambaza maji Nzega

Yobu Ed.jpeg https://ippmedia.com/sw/habari/serikali imetoa-bilioni-12-kusambaza-maji-nzega

Tue, 21 Sep 2021 Chanzo: ippmedia.com

SERIKALI imetoa shilingi bilioni 1.2 kwa ajili ya mradi mkubwa wa maji katika vijiji vinavyoizunguka kata ya Sigiri wilayani Nzega mkoani Tabora.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mratibu wa Taifa wa Mradi wa kurejesha ardhi iliyoharibika na kuongeza usalama wa chakula katika maeneo kame ya Tanzania (LDFS)kutoka katika Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Yobu Kiungo, wakati akikabidhi hati za kimila kwa wananchi wa kata hiyo.

Amesema kwamba fedha hizo zitatumika katika kazi mbalimbali za kutambua na kufanya upembuzi yakinifu kwa vyanzo vya maji na Teknolojia  itakayotumika katika uvunaji wa maji.

Amesema hatua nyingine ni uchimbaji wa malambo matatu, visima virefu sita na bwawa moja ili kuwapunguzia tatizo la maji ya wananchi na mifugo.

Kiungo amesema kuwa wananchi wanatakiwa kupata mafunzo ya kusimamia mashamba darasa kwa wawezeshaji kutoka katika vikundi 21 vyenye washiriki 111 walipewa mafunzo ya kilimo, misitu, mifugo na jinsia .

Amesema kuwa  vijiji ambavyo vitakavyonufaika na mradi huo ni Sigiri, Bulunde, Bulambuka, Lyamalangwa na Iboja.

Awali Mratibu wa maradi huo wilayani Nzega Hassani Mtomela, amesema kwamba wanakusudia kutoa mafunzo ya shamba darasa kwa wakulima kuhusu kilimo hifadhi na mbinu bora za kilimo rafiki kwa mazingira.

Amesema mafunzo hayo yataenda sambamba na kuwasaidia wakulima katika upatikanaji wa mbinu bora za kilimo na pembejeo kwa wakulima katika mashamba darasa yatayoanzishwa.

Wakulima, wafugaji na wananchi watapaitiwa mbinu rahisi ya uvunaji maji na ukarabati au uchimbaji wa mabwawa ya kuhifadhi maji kwa ajili ya kilimo, mifugo na matumizi ya jamii. 

Halmashauri ya Wilaya ya Nzega mkoani Tabora ni moja kati ya halmashauri tano za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinazotekeleza mradi wa kurejesha ardhi iliyoharibika na kuongeza usalama wa chakula katika maeneo kame Tanzania.

Naye Meneja Kanda ya Kati Suzana Mapunda, kutoka Tume ya Taifa ya Mipango na Usimamizi Bora wa Ardhi amesema kwamba kwa kushirikiana na Tume ya Mipango Ardhi ya Zanzibar watawezesha kazi   ya kuwajengea uwezo na kuwashirikisha katika upangaji wa matumizi ya bora ya ardhi.

Hata Hivyo Mkuu Wa Wilaya Ya Nzega mkoani hapa ACP Advera Bulimba, amesema Serikali inatarajia kuchimba visima sita na kukarabati mabwawa madogo matatu na kuchimba bwawa jipya moja.

Amesema kwamba yYote haya ya tafanyika katika Kata ya Sigili kwa ajili ya matumizi ya nyumbani, mifugo na kilimo.



Amesema mpaka sasa Serikali imeshatoa jumla ya shilingi 261,004,590/= kwa ajili ya uchimbaji wa visima sita katika vijiji vya Bulambuka, Lyamalagwa na Bulende.

Aidha, amesisitiza kuwa kwa mwaka huu wa fedha Serikali itatoa fedha kwa ajili ya ukarabati na uchimbaji wa mabwawa.

Ameongeza kusema kwa kuipongeza Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kuona umuhimu wa kuleta mradi huu,Naipongeza Tume ya mipango ya matumizi Bora ya ardhi, Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega.
Chanzo: ippmedia.com