Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali imetenga Sh40 milioni kuboresha lishe Kilindi

Lishepicrrf Serikali imetenga Sh40 milioni kuboresha lishe Kilindi

Sat, 30 Oct 2021 Chanzo: mwananchidigital

Serikali imeombwa kuangalia uwezekano wa kuongeza vyanzo vingine vya mapato kwa ajili ya bajeti ya lishe badala ya kusubiri chanzo kimoja cha mapato ya ndani ya Halmshauri husika.

Ombi hilo limetolewa na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Dk Daniel Chochole wakati Akizungumza Mwananchi Digital kuhusu hali ya lishe katika Wilaya hiyo.

Dk Chochole amesema kuwa endapo Serikali itaongeza vyanzo hivyo vya mapato vitasaidia katika kutekeleza afua mbalimbali za lishe ili waweze kutengeneza afya bora za watoto wenye umri chini ya miaka mitano katika makuzi yao.

Mganga Mkuu huyo amesema kumekuwa na changamoto Katika utekelezaji wa afua mbalimbali za lishe kutokana na kutegemea makusanyo kutoka katika vyanzo vya halmshauri.

" kwasasa tumekuwa tukitumia bajeti za lishe kutoka katika vyanzo vya mapato vya halmashari"amesema Chochole.

Kwa upande wake Kaimu Mratibu wa Lishe wilayani Kilindi, Fikiri Adam ameeleza kuwa kwa mwaka wa fedha 2020/2021 Serikali imetenga Sh40 milioni kwa ajili ya utekelezaji wa afua mbalimbali za lishe wilayani humo.

Hata hivyo lishe bora na huduma zingine za msingi kama elimu na afya ni haki ya kila mtoto kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, lakini mara nyingi mamilioni ya watoto hukosa haki hiyo hususani lishe bora kutokana na sababu mbalimbali. UNICEF inasema hali hiyo inaweka afya za watoto hatarini.

Chanzo: mwananchidigital