Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali haihusiki na bomoabomoa Kivule - DC Ilala

Serikali Haihusiki Na Bomoabomoa Kivule   DC Ilala Serikali haihusiki na bomoabomoa Kivule - DC Ilala

Fri, 10 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo amesema zoezi lililofanyika kata ya Kivule, Bomoabomoa vibanda vya biashara Serikali hawahusiki na kitendo kilichofanyika cha kihuni.

Mkuu wa Wilaya Edward Mpogolo alisema hayo wakati wa ziara yake kata ya kivule kwenda kuwapa pole wafanyabishara wamachinga zaidi ya 37 waliovunjiwa vibanda vyao na kundi la wahuni.

“BOMOABOMOA VIBANDA VYA BIASHARA KIVULE ni kitendo kilichofanyika cha kiuni Jeshi la Polisi Wilaya ya Ilala alijatuma askari wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam ajatuma Askari Mgambo wake wala Mbunge wa Ukonga Jery Silaa viongozi wote wa Serikali wametoa pole jambo hilo," alisema Mpogolo.

Mkuu wa wilaya Edward Mpogolo, alimpongeza Diwani wa Kata ya Kivule Nyasika Getama, kwa taarifa za haraka ambazo amewasirisha wilayani ambapo Mkuu wa wilaya Edward Mpogolo amesema kuna kundi limemzunguka Diwani wa kata ya Kivule Nyasika Getama na kufanya vitendo vya kihuni.

Aidha Mpogolo alisema kutokana na tukio hilo la Bomoabomoa haramu kuvule Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Ilala wameunda tume ya kufanya uchunguzi waliohusika wakibainika watakamtwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria

Katika hatua nyingine Mkuu wa wilaya Mpogolo alisema eneo lililotengwa kwa ajili ya soko la KIVULE sio rafiki na mkataba wa soko la KIVULE ni wa kitapeli ambapo Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Jomary Mrisho Satura na wataalam wake watakuja kuupitia upya mkataba huo na Serikali itatoa pesa kwa ajili ya ukarabati soko hilo ili liweze kutumika na wafanyabishara hivyo wafanyabishara waendelee kufanya biashara katika maeneo yao ya awali amna mtu atakaye wasumbua Serikali ya ni sikivu.

Alishangazwa na viongozi wa Serikali yetu kutumika vibaya ambapo alisema viongozi wa namna hiyo wanamtia mashaka katika uongozi kwani kiongozi bora anajali shida na matatizo ya wananchi.

Alisema Halmashauri ya jiji hawakuvunja vibanda hivyo kivule Serikali inawapenda ,mkuu wa mkoa Dar es Salaam, Mkurugenzi wa jiji na Mbunge wa Jimbo la Ukonga wote wanawaoenda wafanyabishara wa kivule waendelee kuiamini Serikali yao ya awamu ya sita ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan

Diwani wa kata ya Kivule Nyasika Getama alisema katika tukio hilo umefanyika unyama mkubwa wananchi wake wameibiwa vitu mbali mbali Mali na pesa zao wakati Bomoabomoa ya vibanda vya biashara ikifanyika ambapo inadaiwa magari ya Serikali yalitumika ambapo pia kundi hilo limedai litarejea tena kuwabomolea.

Diwani Nyasika Getama alisema jumamosi November 7 mwaka huu kuamkia Jumapili Novemba 8 vibanda 37 vilibomolewa vya wafanyabishara wa kivule ambao wanajitafutia mahitaji yao ya kila siku.

Kaimu Mwenyekiti wa wafanyabishara Kivule Yusuph Salehe alisema idadi ya wafanyabishara wa eneo hilo 37 vibanda vilivyovunjwa 24 wamevunja na kudaiwa kuiba vitu vya thamani ikiwemo fedha taslimu katika maduka ya kubadirisha fedha, feni, Kompyuta na vitu mbali mbali.

Kaimu Mwenyekiti Yusuph Salehe alisema kwa sasa mara baada kutokea hasara hiyo wamekosa mitaji ya biashara na wengine wapo katika mikopo ya marejesho maisha yamekuwa magumu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live