Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali Yakiri Kukosa Fedha Ujenzi Barabara ya Morogoro - Tanga

Bunge.png?fit=676%2C426&ssl=1 Serikali Yakiri Kukosa Fedha Ujenzi Barabara ya Morogoro - Tanga

Tue, 6 Apr 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Serikali ya Tanzania imekiri kukosa bajeti ya ujenzi wa kiwango cha lami barabara ya Kilindi-Iyogwe hadi Gairo yenye urefu wa kilomita 115.7 na badala yake itaendelea kutenga bajeti kwa ajili ya kufanya matengenezo mbalimbali ili kuhakikisha inaendelea kupitika vizuri majira yote ya mwaka.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumanne Aprili 6, 2021 mjini Dodoma na naibu waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Godfrey Kasekenya wakati akijibu swali la mbunge wa Kilindi, Omary Mohamed Kigua aliyehoji ni lini Serikali itajenga kwa kiwango cha lami barabara hiyo kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads).

Akijibu swali hilo katika kikao cha nne cha Bunge la Bajeti linaloendelea, Kasekenya amesema kutokana na ufinyu wa bajeti kwa sasa Serikali haijapata fedha za kuanza ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami. Barabara hiyo inaunganisha mikoa ya Tanga na Morogoro kupitia wilaya ya Kilindi na Gairo.

Chanzo: globalpublishers.co.tz