Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali Simiyu kuunga juhudi uwekezaji Airtel

3a20ba169c0312d06cee4534d2211f84 Serikali Simiyu kuunga juhudi uwekezaji Airtel

Sun, 10 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MKOA wa Simiyu umeipongeza kampuni ya mawasiliano ya Airtel kwa uwezekazaji wake mkubwa mkoani huo huku ukiahidi kuendela kuunga mkono uwezekaji huo.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Miriam Mmbanga, alisema hayo mwishoni mwa wiki katika uzinduzi wa minara ya 4G ya kampuni ya Airtel mkoani humo.

“Kampuni ya mawasiliano ya Airtel Tanzania iko kwenye mkakati wa kuboresha huduma zake ili ziendelee kuwafikia Watanzania hasa kwa maeneo ya vijijini. Hapa mkoani Simiyu wametumifikia na leo wamewasha minara yao ya 4G pamoja na kufungua maduka mapya ya Airtel Money Branches,” alisema Mmbanga.

Akaongeza: “Sisi viongozi wa mkoa tunaahidi kulinda uwekezaji huu ili uwe na tija kwa wananchi wetu.”

Alisema, kampuni za kibiashara mara nyingi huangalia maeneo yenye kurudisha faida kabla ya kuanza kuwekeza kwa sababu uwekezaji ni kama huu ni gharama Kubwa.

“Tunatoa shukrani za dhati kabisa kwa sababu maeneo kama haya ya kwetu yamekuwa hayapewi kipaumbele kwenye uwekezaji” alisema Mmbanga.

Alisema, uwekezaji wa Airtel umekuja na faida kwani wafanyabiashara, wakulima na wachimbaji wa madini sasa watakuwa na uhakika wa kutunza fedha zao kwa usalama kwa kutumia huduma ya Airtel Money.

“Ni kweli maeneo mengi ya mkoa wa Simiyu hayajafikiwa na huduma za kibenki. Kampuni ya Airtel kwa sasa imefanikiwa kupeleka huduma zake zote hadi vijijini. Naomba wananchi watumie huduma za Airtel Money ili kutunza fedha na hii itasaidia kuepukana na wizi’, Mmbanga alisema.

Mkuu wa Mauzo Mkoa wa Simiyu Airtel Tanzania, Godlisten Pallangyo, alisema kampuni ya Airtel Tanzania iko katika mkakati wa muda mrefu kuboresha huduma na kuwafikia Watanzania wengi zaidi na hasa walio vijijini.

“Tunaelewa namna wananchi wanaoishi maeneo ya vijijini wanavyopota changamoto na hasa katika sekta ya mawasiliano. Airtel tumejitolea kuhahakisha changamoto hizo zote zinapata ufumbuzi haraka kama huu,” alisema.

Chanzo: habarileo.co.tz