Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serengeti yakabidhi madarasa 199, chenji yabaki

Hapi Pic Data Serengeti yakabidhi madarasa 199, chenji yabaki

Sun, 16 Jan 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Mkuu wa Wilaya ya Serengeti mkoani Mara, Dk Vicent Mashinji amekabidhi madarasa 119 yaliyojengwa na fedha za Uviko-19 kwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Ally Hapi huku Sh69.9 milioni zikibake.

Akikabidhi madarasa hayo, Dk Mashinji amesema kuwa katika utekelezaji wa mradi huo wamebakiza Sh69.9 milioni kati ya Sh2.38 bilioni walizopokea kwaajili ya mradi huo ambapo pia jumla ya madawati na meza 3,890 yametengenezwa.

Amesema kuwa kukamilika kwa mradi huo kumemaliza tatizo la upungufu wa madarasa katika shule za sekondari wilayani humo na kwamba mradi huo utawezesha wanafunzi wote 6,483 waliofaulu mtihani wa darasa la saba mwaka jana kuendelea na masomo ya sekondari.

"Pamoja na kukabidhi madarasa haya, lakini pia nitumie fursa hii kuwaomba radhi wale wote waliokwazika wakati wa utekelezaji wa mradi wapo watu tulilazimika kuwaweka selo lakini lengo lilikuwa kufikia hatua hii ya leo na sote kwa pamoja tunafurahi mradi umekamilika na jumatatu watoto wote wataanza masomo" amesem Dk Mashinji

Akizungumza baada ya kupokea mdarasa hayo, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Ally Hapi amewataka wazazi kuwapeleka watoto wote shuleni na kwamba endapo mzazi atajaribu kumkatisha mtoto masomo na kumuozesha hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

"Nasikia wapo baadhi yenu wanasema wale watoto wa kike waliomaliza darada la saba sasa wamefikia umri wa kuolewa, ole wake mzazi atakayejaribu kufanya hivyo, niwaombe tu muwaache  hawa watoto Serikali iendelee nao hadi pale itakapokuwa imemalizana nao ndipo mfayanye hayo maamuzi " amesema Hapi

Hapi amewaonya waendesha pikipiki maarufu kama boda boda wanaotumia pikipiki zao kuwarubuni wanafunzi wa kike kisha kuingia nao katika mahusiano ya kimapenzi na kupeleka wanafunzi hao kupata mimba na kuacha shule.

"Kuna wale boda boda domo zege utakuta anamuonyesha mwanafunzi Sh2,000 na kumuuliza hii nini huku wakidai kuwapa lifti kuwapeleka shule sasa ole wako ujichanganye maana huko mitaani wapo wasichana wengi tu ambao mnaweza kuelewana lakini kwa udomo zege wako unawavizia wanafunzi " amesema Hapi

Chanzo: www.mwananchi.co.tz