Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sengerema wapitisha bajeti ya Sh49 bilioni

Bajeti Pic Data Sengerema wapitisha bajeti ya Sh49 bilioni

Tue, 1 Feb 2022 Chanzo: mwananchidigital

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza limeptisha bajeti ya Sh49 bilioni kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023.

Katika bajeti hiyo Halmashauri hiyo inakadiria kukusanya mapato ya ndani ya Sh1.9 bilioni na ruzuku kutoka Serikali Kuu Sh46bilioni na mapato mengine Sh706 milioni.

Akiwasilisha bajeti hiyo kwa niaba ya mkurugenzi wa Halmashauri ya Sengerema Binuru Shekidele, Ofisa Mipango wa Halimashauri hiyo, Samson Ndallo amesema bajeti hiyo ina ongeza la asimilia 4 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka 2021/2022 ya Sh47.1 bilioni.

Wakichangia bajeti hiyo Diwani wa Kata ya Tabaruka, Sospeter Busumabu ameitaka ofisi ya mkurugenzi kuzingatia kupeleka fedha kwenye miradhi ya wananchi ili waweze kupata maendeleo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, Yanga Makaga amesema wamejipanga kuisimamia bajeti hiyo ili ilete tija kwa wananchi.

Chanzo: mwananchidigital