Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sekondari Bwiru kutoa elimu ya ujasiriamali

68074 Pic+bwiru

Wed, 24 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Shule ya Sekondari ya wasichana ya Bwiru  jijini Mwanza imeanza kutoa elimu ya ujasiriamali kwa wanafunzi wake lengo likiwa ni kuwasaidia waweze kujiajiri watakapomaliza masomo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Julai 24, 2019 baada ya ukaguzi wa mradi wa ukarabati na ujenzi wa shule hiyo uliofanywa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, mkuu wa shule hiyo, Mekitilda Shija amesema shirika lisilokuwa la serikali la Kivulini limekuwa likifadhili mafunzo ya sanaa kwa wanafunzi hao.

"Hatununui sare dukani, wanafunzi wetu wana uwezo wa kushona na kuuza  kwa bei ya chini kwa wenzao. Fedha hizo zinatumika kununua vifaa vikiwemo vitambaa na nyuzi za kushona.”

"Tuliamua kukubali mradi huu maana tulitambua umuhimu wake, karibia wanafunzi wote wanaendelea kujifunza fani mbalimbali wakiwa na muda," amesema Shija.

Msimamizi wa somo la sanaa katika shule hiyo, Khadija Abeit amesema mradi huo unajulikana kama Bwiru Industrial Initiative na umesheni zaidi ya wanafunzi 700.

"Wanafunzi wanashona sketi na mavazi mbali mbali pia wanafuma, kuremba na wanaunda skafu za aina nyingi na kuwauzia watu wa nje ya shule," amesema.

Pia Soma

Mmoja wa  wanafunzi, Morini Robert amesema baada ya kushona sketi moja wanauza Sh 3000 badala ya ile ya Sh 8000 inayouzwa katika maduka nje ya shule.

Chanzo: mwananchi.co.tz