Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Samia kuweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara za mzunguko Dodoma

Samia Nassari Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Tue, 8 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Samia Suluhu Hassan kesho ataweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa barabara ya mzunguko wa nje (outer ring road) katika Jiji la Dodoma.

Akizungumza leo Jumanne Februari 8, 2022, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka amesema shughuli hiyo itafanyika katika eneo la Makutopora (Veyula) kesho Jumatano.

“Ataweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa barabara za mzunguko wa nje ya Jiji la Dodoma yenye urefu wa jumla ya kilometa 112.3 inayojengwa kwa kiwango cha lami,” amesema.

Amesema barabara hiyo itakuwa kiungo muhimu na barabara nyingine za Jiji la Dodoma ikiwa imegawanyika kwa makandarasi wawili kutoka nchini China.

Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (Tanroad) mkoani Dodoma Leonard Chimagu amesema ujenzi wa mradi huo umegawanyika katika sehemu mbili ambapo sehemu ya kwanza ni Nala, Veyula, Mtumba hadi Ihumwa kwenye bandari kavu ambayo ina jumla ya kilometa 52.3.

Amesema sehemu ya pili inaanzia bandari kavu ya Ihumwa Matumbulu hadi Nala ambayo ina urefu wa kilometa 60.

“Wakandarasi wameshaanza kazi tangu mwezi Septemba (mwaka jana) na hadi sasa wanafikia wastani wa asilimia nne ya utekelezaji wake na tunatarajia watamaliza kazi kwa muda uliopangwa na kiwango kinachotakiwa,”amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live