Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Salma Kikwete atoa neno kwa madiwani Mbeya

Salma Pic Data Salma Kikwete akiwa na Spika wa Bunge, Dkt.Tulia Ackson jijini Mbeya

Mon, 28 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mke wa Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete, Salma Kikwete amewataka madiwani wa Jiji la Mbeya kutumia fursa ya uwepo wa muhimili wa Bunge kuwasilisha hoja za kuleta maendeleo ya utekelezaji wa miradi na kuepuka tofauti.

Salma ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mchinga Mkoa wa Lindi amesema hayo leo Jumatatu, Februari 28, 2022 alipoungana na Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya Mjini, Dk Tulia Ackson wakati akikabidhi mifuko 200 ya Saruji katika Shule ya Sekondari Itezi Jijini Mbeya na huku akichangia Sh500,000 zilizotolewa na wananchi wa Jimbo la Mchinga.

''Nimekuja kuungana na Spika wa Bunge kutokana na namna anavyojitoa na kujituma katika jamii hivyo niwasihi madiwani mumtumie vizuri ili Jimbo la Mbeya liweze kupiga hatua zaidi ya maendeleo hususan katika Sekta ya elimu '' amesema

Amesema kuwa kwa nafasi aliyonayo ni fursa pekee kwa madiwani kumtumia Dk Tulia na kwamba ujio wake ni fursa ambayo italeta tija na msukumo wa hali ya juu katika kuboreshwa kwa miradi ya maendeleo ya wananchi.

Kwa upande wake Dk Tulia amesema kuwa amekuja Mkoa wa Mbeya kwa mara ya kwanza baada ya kuapishwa kuwa Spika na kipaumbele chake cha kwanza ni elimu.

''Nimekuja na kipaumbele vingi lakini kwa sasa naanza na sekta ya elimu ili Mkoa wa Mbeya uwe wa mfano wa kuigwa kutoka mikoa mingine Tanzania kuja kujifunza namna miundombinu itakavyoboreshwa kisasa '' amesema. Amesema kuwa lengo lake ni kuona watoto wote wenye umri wa kwenda shule wapate elimu kuanzia awali mpaka ya elimu ya Juu.

Diwani wa kata ya Itezi, Shambwee Shitambala ameomba Dk Tulia kuwaboresha miundombinu ya barabara ambayo ni changamoto kwa wanafunzi mvua zinapokuwa zinaonyesha .

Chanzo: www.tanzaniaweb.live