Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sakata wananchi, Serikali eneo la KIA lachukua sura mpya

Kia Pichjnk Sakata wananchi, Serikali eneo la KIA lachukua sura mpya

Mon, 17 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baadhi ya wakazi wa vijiji vinavyozunguka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kilimanjaro (KIA) wamekusanyika kupinga kauli iliyotolewa na Serikali ya Mkoa wa Kilimanjaro kuwa mgogoro kati yao na uwanja wa ndege umemalizika wakati bado shauri la mgogoro huo bado likiwa mahakamani.

Wakizungumza leo April 17, 2023 wananchi hao wamesema taarifa iliyotolewa na Serikali ya Mkoa wa Kilimanjaro imewapa wasiwasi mkubwa kwasababu kufanya hivyo ni sawa na kuingilia muhimili wa mahakama wakati shauri la mgogoro huo bado lipo mahakamani na halijamalizika.

Mmoja wa wakazi wa vijiji hivyo, Jacob William amesema kesi ipo mahakamani lakini cha kushangaza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu katika taarifa yake aliyoitoa siku ya maadhimisho ya miaka miwili ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, alisema mgogoro huo umemalizika jambo ambalo sio la kweli.

Nae Lucas Kilimbei, amesema kesi ipo mahakamani lakini cha kushangaza Mkuu wa Mkoa anatangaza kuwa mgogoro umemalizika huku kesi ikiwa iko mahakamani.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu, amesema kati ya wananchi 1,700 wa eneo hilo, wananchi tisa pekee ndio wanapinga na kwamba wameenda mahakamani kufungua kesi.

Amesema wananchi wengi walikubali kuhama na kwamba wananchi hao wanasubiri fidia ila watapisha eneo hilo ambalo ni la uwanja wa ndege huku akisema wananchi ndio walivamia eneo hilo ila kutokana na uwekazaji Serikali imeona iwafidie ili wapishe eneo hilo.

Mgogoro baina ya vijiji nane na uwanja huo wa KIA umedumu kwa zaidi ya miaka 20, na kati ya Novemba na Desemba mwaka jana Serikali iliweka vigingi kwenye mpaka wa uwanja huo na kutathimini nyumba za wanavijiji wanaodaiwa kuvamia uwanja huo.

Wanavijiji tisa walifungua shauri Mahakama Kuu ya Tanzania (Moshi) kupinga hatua hiyo na Februari 9, 2023 mahakama ilikubali waleta maombi kufungua shauri la msingi. Hata hivyo Mahakama ilitoa amri kuwa wananchi hao waendelee na maisha yao hadi shauri la msingi litakapotolewa uamuzi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live