Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Safari za New MV Victoria zaanza kwa kishindo, yatia nanga Bukoba mapema leo

42f26b478ae17e1c5c8de70882ff2c22 Safari za New MV Victoria zaanza kwa kishindo, yatia nanga Bukoba mapema leo

Mon, 17 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MKUU wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jeneral Marco Gaguti ameongoza wakazi wa manispaa ya Bukoba na viunga vyake katika mapokezi ya Meli New MV Victoria iliyofanya safari yake ya kwanza kutoka Mwanza.

Akizungumza mapema leo baada ya meli hiyo kutia nanga kwenye bandari Bukoba, Mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa wakazi wa mkoa wa Kagera wanapaswa kujivunia jitihada za Serikali za kuhakikisha huduma za usafiri zinarejea kati ya miji hiyo miwili kwani imelenga kuiua uchumi wa wananchi na kurahisisha mawasiliano.

"Ujio wa meli hii utaongeza ajira zaidi ya 400 na kupunguza gharama za usafirishaji mizigo kutoka Mwanza na hata kwa wafanyabiashara wa mikoa ya jirani watakaotumia meli hiyo kupitia bandari za Mwanza na Bukoba," alieleza.

Aidha Gaguti amewaomba wananchi wote kutumia fursa hiyo kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya Tano katika ukuaji wa uchumi na maendeleo lakini pia kujishughulisha ili kuongeza kipato binafsi.

Meli hiyo ina hiyo ina uwezo wa kubeba abria 1,200 na tani 200 za mizigo.

Chanzo: habarileo.co.tz