Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Safari za Dar-Mtwara zarejea

Dar   Mtwaraa Safari za Dar-Mtwara zarejea

Fri, 10 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Safari za Dar es Salaam kwenda Mtwara baada ya kukwama kwa siku sita, hatimaye safari hizo zimerejea baada ya kufanyika matengenezo ya Daraja.

Safari hizo zilisimama kutokana na kukatika kwa njia ya kuelekea Mikoa ya Lindi, Dar es Salaam na eneo la njia ya nne (Mikereng’ende).

Magari ya mizigo, mabasi na magari mengine madogo yaliyokwama kwa siku hizo kuelekea mikoa hiyo yameanza kuruhusiwa kuendelea na safari zake.

Hatua hiyo imechukuliwa jana Mei 09, mara baada ya kukamilisha urejeshaji wa mawasiliano katika maeneo ya Mikereng’ende, Songas na Somanga ambayo yalikatika kutokana na Mvua zilizonyesha na kuambatana na Kimbunga Hidaya.

Akisimamia zoezi hilo, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack amewataka wasafiri, wasafirishaji na watumiaji wengine wa barabara kusafiri kwa tahadhari ambapo maeneo mengine yanaendelea na matengenezo.

“ Naipongeza Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zilizofanyika ndani ya muda mchache na leo (jana) tunashuhudia magari yaliyokwama yameruhusiwa kuendelea na safari”,

Kazi ya urejeshaji wa miundombini ya barabara ya Lindi - Dar es Salaam eneo la Nangurukuru ipo katika hatua ya ukamilishaji chini ya usimamizi wa Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa na Timu ya Wataalam kutoka Wizara ya Ujenzi na Wakala ya Barabara (TANROADS).

Baada ya matengenezo hayo Wananchi wameishukuru Serikali kwa kurejesha mawasiliano ya barabara hiyo kwa vipande na kuweza kuruhusiwa baada ya siku sita kukwama katika barabara hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live